'Milele katika mioyo yetu,'Zari Hassan atembelea kaburi la marehemu mumewe

Angetimiza miaka 46 mnamo Desemba 12 mwaka huu kwani ilikuwa siku yake ya kuzaliwa.

Muhtasari
  • Zari alizaa watoto wake watatu wa kwanza na marehemu mfanyabiashara wa Uganda Ivan Semwanga.

Zari Hassan yuko Uganda na akiwa huko, ametembelea kaburi la marehemu mume wake; Ivan Semwanga.

Akitumia ukurasa wake wa Instagram alimueleza mumewe jinsi wanavompeza.

"Tuna kupeza sana,"Zari aliandika.

Katika chapisho lingine, aliandika "Milele katika mioyo yetu."

Zari alizaa watoto wake watatu wa kwanza na marehemu mfanyabiashara wa Uganda Ivan Semwanga.

Mkubwa ana miaka 19 na wengine wawili ni vijana.

Alifariki Mei 2017 na kuzikwa kijijini kwao Nakaliro, Uganda. Angetimiza miaka 46 mnamo Desemba 12 mwaka huu kwani ilikuwa siku yake ya kuzaliwa.

Akitangaza kifo chake wakati huo, Zari aliandika;

"Mungu anawapenda walio special na ndivyo ulivyokuwa na nadhani ndio maana alikutaka wewe mwenyewe. Umegusa na kusaidia maelfu, ulifanya maajabu nakumbuka uliniambia "life is too short Zee let me live it. kwa ukamilifu”, saa hii ya giza sana inaleta maana kwa nini uliniambia maneno hayo kila mara.” Kwa wana wako, ulikuwa shujaa wa aina fulani.Yeyote ambaye amewahi kuwa mbele yako anajua ulivyokuwa mtu wa haiba. . Utakumbukwa na kukumbukwa kwa njia nyingi sana. Ulikuwa IVAN MKUU!"

Zari amewalea wanawe na Ivan na wa Diamond pamoja bila kuwabagua.