Tanzia:Msanii Nazizi ampoteza mwanawe,akifichua aliaga siku ya Krismasi

Baadhi ya Wakenya waliopata habari kuhusu mkasa huo walituma risala zao za rambirambi kwa Nazizi kwenye mitandao ya kijamii

Muhtasari
  • Alikuwa nchini Tanzania pia kutumbuiza ambayo aliifanya Desemba 24, kulingana na bango alilorusha kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.
NAZIZI
Image: NAZIZI/INSTAGRAM

Mwanamuziki na mtangazaji wa redio Nazizi Hirji anaomboleza baada ya mtoto wake wa miaka mitatu kuanguka na kufariki akiwa likizoni jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Jazeel alianguka kutoka ghorofa ya nne ya hoteli waliyokuwa wakiishi Jumatatu na kufa.

Polisi wa eneo hilo walisema mtoto huyo alikuwa na mzazi na alikuwa amelala. Mzazi alimwacha mtoto amelala na kutoka nje hadi mapokezi ya hoteli hiyo ili kuweka nenosiri lake la wifi.

Mwili huo ulisafirishwa hadi Nairobi kupitia mpaka wa Namanga. Alizikwa siku ya Jumanne.

Baadhi ya Wakenya waliopata habari kuhusu mkasa huo walituma risala zao za rambirambi kwa Nazizi kwenye mitandao ya kijamii

Alikuwa nchini Tanzania pia kutumbuiza ambayo aliifanya Desemba 24, kulingana na bango alilorusha kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Katika taarifa iliyosambazwa na Nazizi kwenye mitandao ya kijamii, Jazeel alifariki katika ajali hiyo katika hoteli walimokuwa wakiishi.

"Tulipoteza roho hii changa katika ajali mbaya katika hoteli ambayo familia ilikuwa inakaa," taarifa hiyo ilisoma kwa sehemu.

"Utupu ulioachwa na kupoteza hauwezi kupimika, na maumivu hayawezi kuvumilika," Nazizi alisema.

Mwimbaji aliomba faragha huku familia ikiomboleza Jazeel.

"Tunaomba huruma na uelewa wako kwa heshima ya hitaji lao la amani wakati huu wa maombolezo."