Mungai Eve azungumzia uvumi wa kuachana na Director Trevor, aahidi kuelezea yote!

Hivi majuzi Trevor aliibuka akisema kwamba mwaka huu ata adopt mtoto wa kiume, katika kile wengi walihisi ni baada ya kutamauka kuzaliwa mtoto na Eve.

Muhtasari

• Eve akionekana kuwa na ufahamu kuhusu kil kinachoendelea baina yao, alimjibu shabiki mmoja kwamba hivi karibuni atalizungumzia suala hilo.

Image: INSTAGRAM// MUNGAI EVE

YouTuber Mungai Eve hatimaye amevunja kimya kuhusu uvumi unaoenezwa mitandaoni kwa siku ya pili sasa kwamba yeye na mpenziwe Director Trevor wamebwagana.

Eve alivunja ukimya huo katika ukurasa wake wa Instagram katika chapisho moja la matangazo na kampuni moja ya mawasiliano humu nchini.

Licha ya kuchapisha tangazo hilo la kibiashara, mashabiki wake hawakuzangatia maudhui ya tangazo lakini walijikita kwenye kipengele cha kutoa maoni na kumsakama na maswali wakimtaka kujibu kama ni kweli wameachana au ni uvumi tu usio na ufizi kishikilizi cha meno.

Hii ni baada ya Mungai kuzifuta picha zote za Trevor katika ukurasa wake wa Instagram naye Trevor kujibu mipigo kwa kuzifuta zote za Mungai.

Eve akionekana kuwa na ufahamu kuhusu kil kinachoendelea baina yao, alimjibu shabiki mmoja kwamba hivi karibuni atalizungumzia suala hilo.

“Kwanza tuconcentrate na saf,” Mungai alimwambia na kumwambia zaidi shabiki mwingine kwamba angeshughulikia uvumi huo.

"Coming up next," aliahidi.

Wapenzi hao wamekuwa pamoja kwa kipindi cha Zaidi ya miaka 5 lakini hawajawahi kuwa na mtoto, jambo ambalo limekuwa likiwaweka chini ya shinikizo mara kwa mara kutoka kwa mashabiki wao.

Mashabiki wamekuwa wakimtaka Eve kumzalia Trevor kama ishara ya kumuonesha mapenzi ya kweli huku wengine wakihisi huenda Trevor ataachwa tu kwenye mataa ya mrembo huyo wakihisi kwamba kwa kuchelewesha kumzalia maana yake ni kuwa pengine hana mipango ya muda mrefu na yeye katika siku zijazo.

Hata hivyo, kufuta picha za kila mmoja kulikuja saa chache tu baada ya Trevor kuibuka akisema kwamba mwaka huu ata adopt mtoto wa kiume, katika kile wengi walihisi ni baada ya kutamauka kuzaliwa mtoto na Eve.