Pritty Vishy akutana na Stevo Simple Boy, ambembeleza ampe salamu kupitia hug (video)

“Kwani ni vibaya kusalimu Ex, ama ni mpenzi wako mpya alikukataza usisalimie Pritty, hutaki stori zangu hata salamu hutaki,” Pritty alimfokea Stevo baada ya kujongea karibu naye kando ya kochi.

Muhtasari

• Baada ya kuketi kwenye kochi, Stevo Simple Boy alijikunyata kama mtu ambaye hataki maneno na mtu kabla ya Vishy kumkurupukia kwa swali kwamba hatimaye ameamua kumfuata kumsalimia.

Stevo akutana na Pritty
Stevo akutana na Pritty
Image: Hisani

Kwa mara ya kwanza maEx Stevo Simple Boy na Pritty Vishy wamekutana katika mazingira tatanishi na kuzua gumzo mitandaoni.

Katika video moja ambayo inazidi kuzungushwa mitandaoni, Stevo Simple Boy aliongozana na wanaume wengine wawili na kuenda katika kileckilionekana kuwa nyumba anamoishic Pritty Vishy.

Baada ya kuketi kwenye kochi, Stevo Simple Boy alijikunyata kama mtu ambaye hataki maneno na mtu kabla ya Vishy kumkurupukia kwa swali kwamba hatimaye ameamua kumfuata kumsalimia.

Hata hivyo, Stevo aliendelea kukaa kimya huku wanaume alioongozana nao wakibwabwaja kwamba Stevo si yeye ana shida bali ni mmoja kati ya hao wawili.

Baada ya kuwasalimia wote, ilibakia zamu ya Stevo lakini akakataa kumsalimia na vijana wale wakamshauri pengine amtake kumkumbatia kwa sababu Stevo alikuwa amekataa salamu ya mkono.

Vishy alianza kumbembeleza Stevo kwa maneno mazuri akimtaka kumsalimia, ikiwemo kumuita mpenzi.

“Mpenzi wangu mbona hutaki kunisalimia, mpenzi wangu salamu ni za Mungu tu naomba nisalimie. Si usimame uni hug,” Pritty Vishy alisema huku akiwa amemnyooshea Stevo mkono bila mafanikio.

Baada ya bembeleza zake kugonga kwenye masikio ya kisiwi, wale vijana walimtaka kupotezea tu wakimshauri kuwa yeye yuko kwenye mahusiano mengine.

“Kwani ni vibaya kusalimu Ex, ama ni mpenzi wako mpya alikukataza usisalimie Pritty, hutaki stori zangu hata salamu hutaki,” Pritty alimfokea Stevo baada ya kujongea karibu naye kando ya kochi.

Wawili hao waliachana mwaka 2022 baada ya kutupiana cheche za maneno ya kashfa na tangu hapo kila mmoja amekuwa akimchafua mwenzake katika mahojiano pindi tu swali kumhusu linaporushwa upande wake.