Muigizaji Nyaboke awashangaza wengi akifichua mwanawe wa kwanza amefikisha miaka 19!

Muigizai huyo mwenye umri wa miaka 39 aliwashangaza wengi kufichua kwamba mtoto wa ujana wake ametimiza umri wa miaka 19 Jumamosi Januari 6.

Muhtasari

• Nyaboke ambaye ana umri wa miaka 39 alimwandikia ujumbe mtamu bintiye akimtakia kila la heri.

Gloria Nyaboke Moraa na bintiye
Gloria Nyaboke Moraa na bintiye
Image: FACEBOOK

Aliyekuwa muigizaji wa kipindi cha Tahidi High kwenye runinga ya Citizen, Nyaboke Gloria amewashangaza wengi baada ya kufichua kwamba bintiye kifungua mimba amefikisha umri wa miaka 19.

Nyaboke ambaye kizazi cha sasa kinamjua Zaidi kutokana na skits zake na mchekeshaji Victor Naaman, alifichua haya kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo alichapisha picha yake akiwa amekumbatiana na bintiye.

Katika chapisho hilo, babamama huyo wa marehemu aliyekuwa mkufunzi wa timu ya raga ya Kenya, Benjamin Ayimba alisema kwamba ana furaha kubwa kumuona mwanawe anaingia katika raundi ya mwisho ya kuumalizia utineja, akisema kwamba huyo ndiye alikuwa mtoto wa ujana wake.

Nyaboke ambaye ana umri wa miaka 39 alimwandikia ujumbe mtamu bintiye akimtakia kila la heri katika safari ya maisha yake kwani yeye kama mama hakuna fahari kubwa anakayojivunia kama kumuona bintiye ametusua kimaisha.

“Msichana wangu mdogo anatimiza miaka 19 leo, mtoto wa ujana wangu. Mungu wangu apanua maeneo yako, afunika hatua zako na akupe haja za moyo wako. Mama anakupenda sana. Mwaka huu siku yako ya kuzaliwa inakuja katika wakati wa kujaribu sana kwetu lakini Mungu yuko. Happy birthday Achieng wangu ️” Gloria Nyaboke alisema.

Mama huyo wa watoto wanne mwaka jana mwezi Septemba wakati alikuwa anasherehea siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 39, alisema yuko tayari kutoka soko ikiwa atapata mwanamume wa kumuoa.

“39 ndio. Mungu amekuwa mwaminifu sana kwangu. Nimeandika na kufuta sana maana nina mengi ya kusema kuhusu huyu binti. Niseme tu Mungu wangu na binadamu wangu wa karibu wamenipata, yaani sina. Nitajiita mwanamke wa chuma na wakati huo huo ua hatari zaidi katika bustani.”

“Niruhusu nijitambulishe tena katika miaka 39 thabiti. Gloria Moraa aka Nyaboke aka Gaidi Mkuu. Na tafadhali, ficha ndugu zako wote wa kiume kwa sababu sasa nimeamua soko ni kama nitatoka sasa. Niko tayari,” alisema.