Niffer apata damu imenyunyizwa katika nyumba aliyomjengea mamake

“Leo mamangu ameamka asubuhi nyumbani na kukuta amefanyiwa haya mambo, yaani hizi ni damu zimezungushwa nyumba nzima." Niffer alisema.

Muhtasari

• “Uchawi upo, lakini Mungu yupo pia,” Niffer aliandika kwenye video hiyo.

Niffer akuta damu nyumbani kwa mamake.
Niffer akuta damu nyumbani kwa mamake.
Image: Instagram

Mjasiriamali Niffer ambaye aliwahi husishwa kuwa katika penzi la Alikiba amepigwa na butwaa baada ya kupata damu imenyunyizwa katika kila kona ya nyumba ambayo alimjengea mamake mzazi.

Kupitia kwa video ambayo aliipakia kwenye Instagram yake kisha baadae kuitoa, Niffer alisema kwamba sasa ndio amaamini kuwepo kwa wachawi lakini pia akasema kwamba Mungu naye yupo.

Mrembo huyo alisema kwamba aliamka asubuhi na kupata matone mengi ya damu yamemwagwa katika kila kona ya nyumba hiyo, jambo ambalo lilitia woga kwa kila mwanafamilia.

“Uchawi upo, lakini Mungu yupo pia,” Niffer aliandika kwenye video hiyo.

“Leo mamangu ameamka asubuhi nyumbani na kukuta amefanyiwa haya mambo, yaani hizi ni damu zimezungushwa nyumba nzima. Kwenye ile nyumba ambayo niliposti hapa kama miezi miwili iliyopita nilimjengea mama,” alisema Niffer.

Hata hivyo mrembo huyo alisema amepata ujasiri baada ya kugundua kuwa Mungu yupo na kumtahadharisha mwenye kufanya hivyo kwamba siku zake za kutumbuliwa hadharani zinakuja.

“Nawakumbusha watu kusali sana kwa sababu tuko katika vita na watu ambao hatuwafahamu, wengine tunacheka nao, tunakula nao, tunawakumbatia, tuko nao kila sehemu lakini ndio watu wanaotufanyia ubaya,”

“Lakini kwa yeyote ambaye anafanya hivi nataka kukuambia kwamba namuamini Mungu peke yake, na mimi namuache yeye ashughulike na wewe kwa sababu yeye ndiye aliyekupa nguvu na uhai kama alivyonipa mimi hapa, lakini huo uhai wako wewe umeamua kuutumia katika kuweka hofu kwenye maisha ya watu, kufanya watu washindwe kuwa na Amani, wahangaike, walie… basi sawa, mimi namuachia Mungu,” Niffer alisema kwa sauti ya kutetereka.