Marioo amfuata Harmonize kwa kolabo ya pili baada ya kumuonya dhidi ya kumlipua Paula

Je, unahisi huo wimbo utakuwa wa namna gani? Ni wa mapenzi, usaliti, maisha ya kawaida kutiana moyo au ni wimbo wa injili?

Muhtasari

• Je, unahisi huo wimbo utakuwa wa namna gani? Ni wa mapenzi, usaliti, maisha ya kawaida kutiana moyo au ni wimbo wa injili?

Harmonize na Marioo kufanya kolabo tena
Harmonize na Marioo kufanya kolabo tena
Image: Facebook

Harmonize na Marioo kwa mara nyingine tena wameonekana studioni katika kile kinasemekana wawili hao wamejumuika pamoja kufanya kolabo.

Endapo taarifa hizo ni kweli, basi hii itakuwa ni kolabo yao ya pili bada ya kolabo ya kwanza ya ‘Naogopa’ kupata ufanisi mkubwa mwaka mmoja uliopita.

Ukurasa wa Instagram wa Konde Gang ulipakia video ya Marioo na Harmonize wakiwa kwenye studio wakirekodi wimbo na kuandika kwamba wawili hao wameamua kuwabariki mashabiki wao kwa mara nyingine tena na ngoma ya pamoja.

“Mnakumbuka hii combo? OMG wanarudi tena,” ujumbe huo ulisema.

Mashabiki wa wasanii hao walisalia na maswali mengi wakijiuliza wimbo huo utakuwa ni wa maudhui gani ikizingatiwa kwamba maisha yao kwa njia moja au nyingine yamepishana katika suala zima la kimapenzi.

Itakumbukwa Marioo kwa sasa ni mpenzi wa Paula, binti wa aliyekuwa mpenzi wa Harmonize Kajala Masanja ambapo kwa urahisi tunaweza tukasema Paula aliwahi kuwa mtoto wa kambo wa Harmonize, hivyo wangekuwa pamoja Marioo angekuwa mkaza mwana wa Harmonize.

Lakini baada ya Harmonize kuachana na Kajala, kilichofuatia ni vichambo na vijembe vya kila aina kutoka kambi zote mbili, jambo ambalo lilimfanya Marioo miezi miwili iliyopita kutoa onyo kali kwa Harmonize dhidi ya kuendelea kumshambulia Paula kwa maneno makali kisa penzi lililovunjika la mamake.

“Mimi sidhani kama shida ya mpenzi wangu na wabaya wake, sawa kwa sasa napendana naye na naweza nikavaa ugomvi wake wowote, lakini binafsi mimi sikutaka iwe hivyo… sasa hivi mtu yeyote yaani, awe nani awe nani, yaani yeyote yule, sasa hivi mchumba wangu keshamalizana na hao watu wote, hana shida na mtu yeyote kaamua kuzingatia tu maisha yake,” Marioo alisema.

“Amegombana sijui na Ex wake wamechambana kishenzi, mimi nimeona nimekausha kwa sababu ilibidi iwe hivyo, hainihusu. Maneno maneno wametupiana huko sijui na aliyekuwa babake wa kufikia nimekausha kwa sababu hayanihusu, mambo yote keshaisha. Sasa hivi mtu yeyote…mtu yeyote akiyatimba sasa hivi, nipo naye, tutaongea na yeye vizuri,” Marioo aliongeza kwa ukali.

Je, unahisi huo wimbo utakuwa wa namna gani? Ni wa mapenzi, usaliti, maisha ya kawaida kutiana moyo au ni wimbo wa injili?