Polisi wa Nigeria waanzisha uchunguzi Davido akituhumiwa kumtishia maisha Tiwa Savage

Tiwa analalamika kwamba baada ya kupiga picha na babymama wa Davido na kuichapisha kwenye instastory yake, Davido alimtumia ujumbe mkali akimtishia maisha na pia kumsimanga kwa maneno ya nguoni.

Muhtasari

• Savage, katika ombi hilo linalosambazwa hivi sasa, alimshutumu Davido kwa kutoa maneno ya dharau.

• Tiwa amedai Davido alimtolea maneno ya kumdhalilisha na chuki pamoja na kumtumia Watu kwa ajili ya kumuonya kwamba awe makini akiwa katika Jiji la Lagos.

Tiwa Savage na Davido
Tiwa Savage na Davido
Image: Facebook

Polisi mjini Lagos, Nigeria wameripotiwa kuanzisha uchunguzi baada ya msanii wa kike Tiwa Savage kudaiwa kumshtaki rafiki yak wa muda mrefu ambaye pia ni msanii, Davido.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka nchini humo, Tiwa Savage aliandikisha ripoti kwa polisi akidai kuwa Davido amekuwa akimsimanga na hata kumtishia maisha yake.

Hii ni baada ya Tiwa Savage kupiga picha na mmoja wa babymama wa Davido, jambo ambalo mkali huyo wa Afrobeats alidaiwa kuchukizwa nalo kupelekea wawili hao kusitisha urafiki wao kwenye Instagram.

Afisa wa Mahusiano ya Umma wa Polisi wa jimbo hilo, Benjamin Hundeyin, alipokuwa akijibu uchunguzi wa gazeti la PUNCH nchini humo siku ya Jumanne, alisema uchunguzi umeanza kuhusu madai hayo.

Alisema, "Ninaweza kukuthibitishia kwamba tumepokea ombi na uchunguzi umeanza."

Savage, katika ombi hilo linalosambazwa hivi sasa, alimshutumu Davido kwa kutoa maneno ya dharau kwa kujibu chapisho ambalo lilijumuisha yeye na Baby mama wa mwimbaji huyo Sophia Momodu kwenye Instagram story.

Tiwa amedai Davido alimtolea maneno ya kumdhalilisha na chuki pamoja na kumtumia Watu kwa ajili ya kumuonya kwamba awe makini akiwa katika Jiji la Lagos, kitu ambacho kinatishia Haki yake ya Maisha, Utu na Faragha Hadi sasa, Davido hajajibu chochote kuhusu tuhuma hizo.

Ombi hilo lilisomeka kwa sehemu, "Tarehe 23 Desemba, niliandika chapisho ambalo lilijumuisha hadithi yangu ya Instagram ya Sophia Momodu- kipengele kwenye Instagram ambacho kinakuruhusu kuweka chapisho kwa masaa ishirini na nne, na MR. DAVID ADELEKE alituma ujumbe kwa meneja wangu ambaye pia ni sehemu ya timu yake ya usimamizi kwamba nisiwe na wasiwasi na kamwe nisiseme neno lolote kwake na kwamba nilikuwa nikimdhihaki, nikimtamkia maneno ya heshima, nia mbaya na ya dharau kwa mtu wangu.”