Stevo Simple Boy: Jamani Dm imejaa vichuna wananiambia aki Stevo uko so hot

“chochwa kabisa na filters bro😂 .” Mtumizi mmoja wa Instagram alimwambia.

Muhtasari

• “Jamani DM imejaa vichuna wananiambia aki Stevo uko so hot,” Stevo Simple Boy alianidka.

• Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo anayejulikana kwa misamiati yake ya kubuni kudai kwamba warembo wamekuwa wakikita kambi katika DM zake.

Stevo Simple Boy
Stevo Simple Boy
Image: Instagram

Kwa mara nyingine tena rapa tevo Simple Boy amedai kwamba warembo wamefurika katika DM zake wakimsifia kutokana na utanashati wake uliopitiliza.

Stevo kupitia Instagram yake akiendelea na michakato ya kupigia debe wimbo wake mpya ‘Vichuna’ alisema kwamba katika DM zake, kila mara anapofungua anaona warembo wakimwambia jinsi anavyowakosha na kuwanyima usingizi.

“Jamani DM imejaa vichuna wananiambia aki Stevo uko so hot,” Stevo Simple Boy alianidka.

Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo anayejulikana kwa misamiati yake ya kubuni kudai kwamba warembo wamekuwa wakikita kambi katika DM zake wakifukuzia kipande cha penzi lake.

Miezi minne iliyopita, Stevo alidai kuwa warembo wa kutoka taifa jirani la Tanzania walikuwa wamefurika kwenye DM zake wakimtaka kimapenzi.

“Vichuna wa Tanzania wamejaza DM yangu wanasema Stevo Simple Boy tafadhali chagua binti mmoja wetu awe mke wako. Nina uhakika sema sasa hivi sina bando ningewaonyesha. Wapo wengi,” alisema Stevo.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wake wanahisi ni njia moja tu alikuwa anatumia kujipigia debe na wimbo wake mpya;

“Ati vichuna wanakushow we ni mali😂” Nairobibuzzke

“Wanakuchocha tafta kazi ufanye....😢” Patoostarman

“chochwa kabisa na filters bro😂 .” Mattoxjackson.