Usipomdanganya mwanamke maana yake ni kwamba hujali hisia zake - Stephen Letoo

Muhtasari

• Kwa mujibu wa Letoo, tabia ya wanaume kudanganya ni kiashiria kikubwa kwamba wanajali na kudhamini hisia za wanawake.

Stephen Letoo
Stephen Letoo
Image: Facebook

Ripota wa masuala ya kisiasa wa runinga ya Citizen TV, Stephen Letoo amezua gumzo katika mtandao wa Facebook baada ya kudai kwamba hulka za wanaume kuwa wadanganyifu haswa katika mahusiano ya kimapenzi ni kwa faida ya wapenzi wao wa kike.

Letoo ambaye amekuwa akijinadi kama msemaji wa wanaume kuelekea sikukuu ya Valentino ambayo pia hutaniwa kuwa ni siku ya kongamano la wanaume, aliwashauri wanawake kwamba wakiona wanaume wao wanawadanganya tafsiri yake ni kuonesha upendo na hisia kwao.

Letoo alisema kwamba mwanamume yeyote ambaye hajawahi mdanganya mwanamke anayempenda basi ni ishara kwamba hana haja na hisia zake.

Kwa mujibu wa Letoo, tabia ya wanaume kudanganya ni kiashiria kikubwa kwamba wanajali na kudhamini hisia za wanawake wanaopwapenda, hivyo wanawake hawafai kununa au kusonya pindi wanapogundua wanaume wao ni waongo au wadanganyifu.

“Mwanaume ambaye hajawahi kumdanganya mwanamke hajali hisia zake,” Letoo alisema katika picha alichopakia akionekana kuzungumza na mtu kwa simu panda la uso likiwa limegubikwa na tabasamu ghaya.

Baadhi ya wanaume walimtania kwamba anamwaga mtama kwa kuku wengi, wakisema kuwa hiyo ni siri tu ambayo inafaa kufichuliwa kwa wanaume pekee wakati wa kongamano lao Februari 14.

“Au ukitaka kubaki single au usioe endelea kusema ukweli kwa mwanamke,” Reagan Jason.

“Men's conference Niko imekaribia ama vipi” Ada Shaks Senteman.

“Amina mheshimiwa mwenyekiti, mafundisho yako hakika yanabadilisha na kuwakomboa wanaume wengi, lazima tukae wataliban na tusiotawaliwa na jinsia iliyozungumza na nyoka.” Kose Kamili.