Zari awazomea slayqueens wanaomuomba pesa kwenye DM, awataka kuacha kufeki maisha

Zari alikanusha kuwa alirithi utajiri kutoka kwa mume wake, akisema kwamba miaka ya nyuma aliwahi fanya kazi 'chafu' zikiwemo kuwa mjakazi wa ndani nchini UK.

Muhtasari

• Pia aliwaonya watu wote wanaoeneza habari za uongo kuhusu yeye kuwa tajiri kwa sababu ya utajiri wa marehemu mumewe, Ivan Ssemwanga.

• Anasema mali yao waliifanyia kazi yote pamoja, na amefanya bidii zaidi kuitunza na kuiboresha.

ZARI HASSAN
ZARI HASSAN
Image: Instagram

Mwanasosholaiti na mjasiriamali maarufu kutoka nchini Uganda, Zari Hassan amechukizwa na tabia ya wasichana slayqueens kujipaisha katika maisha ya kuigiza na badala yake amewataka kujitahidi katika kufanya kazi kujipatia vya kwao.

Katika video ambayo imeenezwa kwenye mitandao ya kijamii, Zari alisema kwamba ni kinaya kupata slayqueen wengi wanatumia kiasi kikubwa cha pesa kila siku kujifurahisha bila ya kuwa na kazi maalum ya kuwaingizia kipato hicho.

Zari alifichua kuwa licha ya kuwa anaishi maisha ya kusisimua na watu wengi wanamtegemea, ameshawahi kufanya kazi "chafu" hadi kufikia hapo alipo kwa sasa.

Alisema amefanya kazi katika kampuni ya sandwich na kama mjakazi wa nyumbani nchini Uingereza hapo awali.

Zari anaamini kuwa unapofanya kazi kwa bidii, kila mtu anaheshimu hustle zako.

Aliwashauri maslay queens wote wanaoendelea kuomba katika DMs kwenda huko na kufanya kitu hata kama ni kuuza mkaa badala ya kuweka viwango ambavyo hawawezi kukidhi.

Pia aliwaonya watu wote wanaoeneza habari za uongo kuhusu yeye kuwa tajiri kwa sababu ya utajiri wa marehemu mumewe, Ivan Ssemwanga.

Anasema mali yao waliifanyia kazi yote pamoja, na amefanya bidii zaidi kuitunza na kuiboresha.

Mama huyo wa watoto watano alikuwa akizungumza katika lugha ya Kiganda kwenye klipu hiyo.