Baba achukizwa na kitendo cha mwanawe kukataa viatu vya shule alivyomnunulia

Baadhi ya watumizi wa mtandao walimuunga mkono mtoto huyo wakisema kwamba viatu vyenyewe vinakaa sura mbaya ambayo inaweza ikawavutia watu wa kumkejeli shuleni.

Muhtasari

• Cha kushangaza ni kwamba baada ya kumkabidhi mwanawe, mtoto huyo alisusa na kuvikataa viatu hivyo bila sababu yoyote, jambo lililompandisha babake jazba.

mtoto akataa viatu vya shule
mtoto akataa viatu vya shule
Image: X

Baba mmoja mwenye hasira amechukua kwenye jukwaa la blogu ndogo ndogo la X kulalamika vikali kitendo cha mwanawe kuvikataa viatu ambavyo alimnunulia kwa ajili ya kwenda shule.

Baba huyo kwa jina @Life_After_18+ alisema kwamba alikwenda sokoni na kuvikuta viatu vilivyovutia jicho lake na kuona kwamba vinamfaa kabisa mwanawe kwa ajili ya kuvaa kwenda shuleni.

Alichomoa pesa zake alizozipata kwa taabu mno kutoka mfukoni na kuvinunua viatu vile kwa bashasha kwamba mwanawe atavipokea kwa mikono mikunjufu.

Cha kushangaza ni kwamba baada ya kumkabidhi mwanawe, mtoto huyo alisusa na kuvikataa viatu hivyo bila sababu yoyote, jambo lililompandisha babake jazba.

“Mwanangu hana shukrani sana! Asubuhi hii alikataa kuvaa viatu hivi vya shule ambavyo nilimnunulia kwa pesa zangu za kazi ngumu 💔” baba mtu alindika.

Hata hivyo, alishuhudia maoni ya kumchukiza hata Zaidi kutoka kwa watumizi wa mtandao huo ambao waliungana na mtoto kuvikataa viatu vyenyewe wakisema kwamba havikuwa na muonekano wa kuvutia kwa mwanafunzi.

“Viatu hivyo vina paji la uso 😅Bora nitembee bila viatu🚮” @CalliePhakathi

 

“Hebu fikiria kwenda shule na hao Vincent Kompany 😂😂😂😂😂😂” @djTshepoGosiame

 

“Njia ya haraka zaidi ya kuwachukua wanyanyasaji katika nafasi yako” I am Kobene alisema.

“Ikiwa baba yangu angeninunulia hizi ningedai mtihani wa baba kwa sababu sio hivyo ni baba yangu.” @DjDukesta

“Simlaumu, hawa ni wabaya kaka. Kwanini umfanyie hivi smh” Mwingine alisema.