Diamond: Wapinzani wangu wanatambia Range Rover ila kwangu ni gari la mwanamke tu!

"Nasikia raha kuona kwamba yaani gari la mwanamke wangu ndilo gari wanalotambia wapinzani wangu. Yaani gari la demu wangu wao ndio gari la kuvimbia,” Diamond alisema.

Muhtasari

• Diamond alisema kwamba si tu kujisikia vizuri ndani ya gari la Zuchu bali pia anafurahi kuona kwamba gari ambalo wapinzani wake wanatamba nalo, kwake linabaki tu kuwa la mpenzi wake.

Harmonize, Alikiba na Diamond
Harmonize, Alikiba na Diamond
Image: Instagram

Bosi wa lebo ya WCB Wasafi, Diamond Platnumz amewashambulia wapinzani wake kimuziki kwa mana ya Harmonize na Alikiba kisa kuringia kumiliki magari aina ya Range Rover.

Katika video ambayo ilipakiwa na Zuchu, mrembo huyo alimrekodi mpenziwe Diamond akiwa anajaribu kuendesha gari lake aina ya Range Rover ambalo alinunua mwaka jana.

Zuchu kisha anasikika akimuuliza Diamond anajisikia aje kuendesha gari la Range Rover na jibu ambalo Diamond alimpa lilionekana kuwa mkuki mkali kwa kambi za Kings Music na Konde Gang.

Diamond alisema kwamba si tu kujisikia vizuri ndani ya gari la Zuchu bali pia anafurahi kuona kwamba gari ambalo wapinzani wake wanatamba nalo, kwake linabaki tu kuwa la mpenzi wake.

“Mpenzi wangu, babe unajisikia aje kuendesha Range, tajiri?” Zuchu alimuuliza.

“Sijisikii raha tu kuendesha Range lakini nasikia raha kuona kwamba yaani gari la mwanamke wangu ndilo gari wanalotambia wapinzani wangu. Yaani gari la demu wangu wao ndio gari la kuvimbia,” Diamond alizidi kusema huku Zuchu akimkomesha kwamba imetosha kwa jibu lake.

Mashabiki wa muziki wa bongo Fleva wakihisi kwamba msanii huyo alikuwa analenga mashambulizi yake kwa wapinzani wake wakuu, Alikiba na Harmonize ambao magari yao ya maana ni Range Rover.

Harmonize amekuwa akivimba na umiliki wa magari ya Landcruiser V8 lakini pia kuwanunulia wapenzi wake magari aina ya Range Rover ambayo kwa kifupi yamegeuzwa kuwa zawadi kwa wanawake wapenzi tu.

Sikiliza video hii hapa upate kujua Diamond alikuwa anamaaniisha kina nani kama wapinzani wake;