Diana Marua afichua muda uliomchukua kufikisha wafuasi milioni moja YouTube

“Haijakuwa rahisi marafiki zangu, ni bidii yenu na kujitolea kwenu. Unajua kuwatafutia maudhui kila wakati sio jambo rahisi." Diana alisema.

Muhtasari

• “Huu ndio ushindi wangu wa kwanza mkubwa kwa mwaka 2024, nawapenda sana watu wangu,” alisema.

Diana B
Diana B
Image: Facebook

Mkuza maudhui kwenye mtandao wa YouTube, Diana Marua amevunja kimya chake, siku chake baada ya kuwa celeb wa kwanza mwanamke kutoka Kenya kufikisha wafuasi milioni moja kwenye jukwaa la video la YouTube.

Marua kupitia jukwaa hilo alishiriki video akifungua simu yake kwa mara ya kwanza na kuenda YouTube kubaini amefikisha wafuasi wangapi.

Yeye alikuwa anadhania amesalia na wafuasi 140 kufikisha milioni moja lakini kwa mshangao alipata tayari ameshahitimu milioni moja, jambo ambalo hakuweza kuliamini na kupiga kelele za furaha.

“Uongo, sijafika, sasa hivi nilikuwa nimebakisha 140,” Diana Marua alisema huku akipokezwa simu kujihakikishia mwenyewe.

Baada ya kuhakiki amefikisha wafuasi milioni moja na kuingia kwenye orodha fupi ya Wakenya maarufu wenye wafuasi kiasi hicho, aliwashukuru mashabiki wake kwa kumshika mkono hadi kufikisha milioni moja.

Msanii huyo wa rap alifichua kwamba imemchukua Zaidi ya miaka 3 kufikisha idadi hiyo kubwa ya wafuasi, na kuwa mwanamke pekee wa Kenya kuwahi kujinafasi miongoni mwa wanaume wachache.

“Timu D hatimaye tumefanikisha, milioni moja tayari. Ahsante sana nawapenda sana. Imenichukua miaka mitatu, miaka mitatu na robo kufikisha wafuasi milioni moja. Nasikia joto kusema kweli. Timu Diana ahsante sana kwa kufanikisha hili.”

“Haijakuwa rahisi marafiki zangu, ni bidii yenu na kujitolea kwenu. Unajua kuwatafutia maudhui kila wakati sio jambo rahisi. Halafu pia shukrani sana kwa watoto wangu, mume wangu na kila mtu ambaye amekuwa nyuma yangu, ahsante sana hata kwa wenye tulianza nao lakini hatukumaliza nao, ahsante sana, timu Diana ndio mwanzo tunaanza tena,” alisema kwa furaha.

Diana alisema kwamba huo ni mwanzo tu wa mafanikio yake ya ushindi kwa mwaka 2024 na kusema kwamba mwaka huu atashinda vitu vingi vikubwa.

“Huu ndio ushindi wangu wa kwanza mkubwa kwa mwaka 2024, nawapenda sana watu wangu,” alisema.