Eric Omondi azungumzia mipango yake na mtoto wa kiume waliyezaa na Jackie Maribe

Hii ni baada ya mke wake Lynne kuingia katika mitandao ya kijamii wiki chache zilizopita na kudai kwa madaha na mikogo kwamba yeye ndiye mwanamke pekee aliye na mtoto na Eric Omondi.

Muhtasari

• Omondi alipoulizwa kuhusu hilo, alimtetea Lynne na kusema kwamba ni mpenzi wake na chochote anachokisema anajiamini kwa hiyo ana maelezo yote.

Jackie Maribe na Eric Omondi walipopatana miezi michache iliyopita.
Jackie Maribe na Eric Omondi walipopatana miezi michache iliyopita.
Image: SIMON KABU

Mwanaharakati Eric Omondi amezungumzia mipango yake ya mwanawe ambaye walizaaa na mwanahabari Jackie Maribe.

Akizungumza na Massawe Japanni katika kituo cha Radio Jambo, Omondi aliweka wazi kwamba kwa sasa yeye ni baba kwa watoto wawili, wa kike na wa kiume kutoka kwa mama tofauti.

Alisema kwamba japo wengi wanamuona kila mara akizungumzia mtoto wake na mke wake Lynne, Omondi alisema kwamba haitoweza kufichika kwamba mtoto wa Jackie Maribe ambaye ni wa kiume pia ni mtoto wake wa damu.

Omondi alisema kwamba japo kumekuwa na baadhi ya mambo hapo nyuma kutokea ikiwemo yeye kudai kwamba alitaka vipimo vya DNA na mtoto huyo ili kumsaidia, Omondi alisema kwamba hivi karibuni atafanya mazungumzo na Maribe ili kuweza kupata njia ya kumlea wamao.

“Yule ni mtoto wangu wa kiume, mimi nina watoto wawili. Mwanangu na Jackie Maribe nitamfundisha, nitamlea, nitaishi na yeye, ni mtoto wangu,” Omondi alisisitiza.

 Hii ni baada ya mke wake Lynne kuingia katika mitandao ya kijamii wiki chache zilizopita na kudai kwa madaha na mikogo kwamba yeye ndiye mwanamke pekee aliye na mtoto na Eric Omondi.

Omondi alipoulizwa kuhusu hilo, alimtetea Lynne na kusema kwamba ni mpenzi wake na chochote anachokisema anajiamini kwa hiyo ana maelezo yote.

Hata hivyo, hakuzungumzia mipango ya harusi yake na Lynne, na kusema kwamba yeye ni mwanamume kamili wa kiafrika ambaye kama tayari ameshapata mtoto na yeye, hilo ni dhibitisho tosha kwamba anampenda na mipango mingine itafuata kadri muda utakavyoruhusu.