Tiwa Savage kujinunulia mkoba wa milioni 23.9 kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa

Msanii huyo atakuwa anafikisha umri wa miaka 44 mnamo Februari 5.

Muhtasari

• Haya yanajiri wiki chache baada ya Tiwa Savage kutengeneza vichwa vya habari aliponunua jumba la kifahari lenye thamani ya Naira 1.7Billion jijini London.

TIWA SAVAGE
TIWA SAVAGE
Image: Facebook

Mwanamke aliyebadili jinsia ambaye mwili wake umejaa tattoos, kutoboa, na marekebisho makubwa, amewashambulia wakosoaji wanaodhani kuwa yeye ni mzazi mbaya kutokana na mwonekano wake.

Malkia wa Afrobeats amegonga vichwa vya habari baada ya kudai kwamba anawazia kujinunulia zawadi nzuri na ghali ya siku yake ya kuzaliwa.

Msanii huyo atakuwa anafikisha umri wa miaka 44 mnamo Februari 5.

Tiwa Savage, mama wa mtoto mmoja anafikiria kutema kima cha dola 147,000 – sawa na shilingi za Kenya milioni 23 kwenye mkoba wa wabunifu katika chapisho jipya kabla ya siku yake ya kuzaliwa.

Haya yanajiri wiki chache baada ya Tiwa Savage kutengeneza vichwa vya habari aliponunua jumba la kifahari lenye thamani ya Naira 1.7Billion jijini London.

Katika gumzo la Whatsapp na rafiki aliyeshirikishwa kupitia hadithi zake za Snapchat, Tiwa Savage alishiriki picha ya begi la kibunifu akimuuliza rafiki yake kama anunue au la kwani siku yake ya kuzaliwa ni baada ya wiki chache.

Tiwa Savage aliandika; “Ninunue au niache. I meannnn siku yangu ya kuzaliwa ni katika wiki chache."

Habari hizi zinajiri wiki chache baada ya kupapurana na aliyekuwa rafiki wake wa karibu, msanii Davido ambaye alidaiwa kumtishia maisha.

Inaarifiwa kwamba Zogo lilianza pale Savage alipopiga picha na kupakia mitandaoni akiwa na babymama wa Davido, jambo lililoonekana kummkwaza mkali huyo wa ‘Unavailable’.

Davido anaripotiwa kuanza kumtumia Savage jumbe za kumtishia maisha jambo lililomfanya mrembo huyo kupiga ripoti katika kituo cha polisi.

Mpaka sasa haijulikani kesi yao iliendelea vipi kwani mara ya mwisho kusikika kwa habari hizo polisi walisema walikuwa wameanzisha uchunguzi dhidi ya Davido na jumbe zake za kumtishia maisha Tiwa Savage.