Wema Sepetu afichua umri wake halisi akisimulia kumbukumbu maalum ya utotoni na Rais Samia

Katika siku za nyuma, kumekuwa na mashaka mengi kuhusu umri wake halisi.ikizingatiwa kwamba amekuwa kwenye tasnia kwa miaka mingi.

Muhtasari

•Wema Sepetu amemsherehekea rais wa nchi hiyo jirani, Samia Suluhu Hassan wakati anaadhimisha miaka 64 ya kuzaliwa kwake.

•Wema alizungumzia jinsi rais Samia alivyompatia zawadi ya thamani sana alipokuwa akifikisha miaka 6 mwaka 1996

akipokea tuzo kutoka kwa rais Samia Suluhu Hassan katika siku za nyuma.
Wema Sepetu akipokea tuzo kutoka kwa rais Samia Suluhu Hassan katika siku za nyuma.
Image: INSTAGRAM// WEMA SEPETU

Muigizaji mkongwe wa filamu bongo na ambaye aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Wema Sepetu amemsherehekea rais wa nchi hiyo jirani, Samia Suluhu Hassan wakati anaadhimisha miaka 64 ya kuzaliwa kwake.

Rais huyo wa sita wa Jamhuri ya Tanzania aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa Jumamosi, Januari 27 na maelfu ya Watanzania walijumuika kumsherehekea.

Katika ujumbe wake kwa kiongozi huyo wa taifa, muigizaji Wema Sepetu alimtaja kama mwanamke jasiri na kumtambua kama mama yake.

“Acha nichukue fursa hii ya thamani kumtakia Heshima, Kiongozi wetu, Mmoja na Pekee, The Iron Lady, Mama Yangu Kipenzi, Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan Kheri ya siku ya kuzaliwa,” Wema Sepetu aliandika siku ya Jumapili asubuhi.

Aliambatanisha taarifa yake na picha kadhaa za kumbukumbu zake na Rais Samia.

“Ndiyo..!! Baada ya foleni ya jana kupungua maana wishes zilikuwa nyingi  sana. Mama nakupenda sana,” aliongeza.

Mpenzi huyo wa mwimbaji Whozu aliendelea kusimulia kuhusu kumbukumbu nzuri yake na rais Samia kutoka enzi za utoto wake.

Wema alizungumzia jinsi mrithi huyo wa hayati rais John Pombe Magufuli alivyompatia zawadi ya thamani sana alipokuwa akifikisha miaka 6 mwaka 1996 na kufichua jinsi anavyopanga kulipa tendo hilo nzuri.

“Labda tu niseme mimi apa nakuthamini na nakupenda. Sasa niwaambie tu kitu kimoja mwenzenu mimi apa Mama Samia alinileteaga my first gold chain on my 6th Birthday back in 1996 nilipofanya My First Birthday Party pamoja na Daddy Sepetu,” Wema Sepetu alisimulia

Aliendela, “Mama na mimi nina mkufu wako wa dhahabu pia nitauleta Ikulu kama Birthday present yako kutoka kwangu.  Hata nisipokupa personally, nitauacha pale reception. Msije kusema najikweza ni true story just so you know. Kazi Iendelee na Itikadi zifatwe na kuzingatiwa.”

Kwa kufichua kuwa alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 6 mwaka wa 1996, hii inathibitisha tu kwamba mwigizaji huyo atakuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 34 mwezi Septemba mwaka huu.. Katika siku za nyuma, kumekuwa na mashaka mengi kuhusu umri halisi.wa muigizaji huyo ikizingatiwa amekuwa kwenye tasnia kwa miaka mingi.