Haikuwa harusi, ilikuwa ni video shoot na yule Omosh alikuwa ni video vixen tu! - Akothee

Akothee alisisitiza kwamba kichwa chake kinaenda darmadaru na hisia za mapenzi pindi anapomuona Nelly Oaks huku akisema kwamba Omosh hakuwa mpenzi bali video vixen tu.

Muhtasari

• Watu walianza kumuuliza kama wamerudiana na Nelly Oaks ambaye wamekuwa wakionekana naye mara kwa mara.

Akothee na aliyekuwa mumewe wake Denis Shweizer
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Kwa mara nyingine tena, msanii Akothee amerejelea kuzungumzia ndoa yake na mzungu Denis Shweizer amayo ilisambaratika miezi minne tu baada ya kufunga harusi ya kifahari.

Akizungumzia kuhusu kuvunjika kwa ndoa hiyo mwishoni mwa wiki jana, Akothee alionekana akiwa na meneja wake wa zamani ambaye pia ni ex wake, Nelly Oaks na kusema kwamba huyo ndiye roho yake inadunda ikimuona.

Akothee alisema kwamba yule mzungu kutoka Uswizi, aliyembatiza kwa jina Mr Omosh wala hakuwa mpenzi wake na kile kilichotokea mwezi wa Aprili mwaka jana haikuwa hafla ya harusi bali ni hafla ya ku’shoot video, mzungu huyo akisimama kama kiwakilishi cha vixen wa video.

"Kichwa changu kinavimba anapokuwa karibu kama unajua unajua@nellyoaks Alifika na chumba changu ona suite yangu ooh zawadi za Valentines zilishuka mapema mno," mjasiriamali huyo wa Akothee Safaris alisema.

Watu walianza kumuuliza kama wamerudiana na Nelly Oaks ambaye wamekuwa wakionekana naye mara kwa mara katika mikao ya ukakasi, na Akothee hakusita kuwajibu ukweli wote kuhusu ndoa ya awali.

“Ni nini kilimpata mumeo mzungu wa Uswizi uliyefunga naye ndoa? nyie hamko pamoja tena?" mtumiaji wa Instagram anayejali, Ella, ambaye anaonekana kutofahamu kilichojiri aliuliza.

"Hiyo ilikuwa ni shoo ya video ambayo alikuwa vixen video iko kwenye YouTube," Akothee alijibu.

Walakini, Ella hakuwa peke yake ambaye hakujua kwani maswali mengi sawa yaliibuka na Akothee alitoa jibu sawa.

"Ilikuwa ni upigaji video sio harusi, kwani hauna bundles," alijibu mwingine.

A

akothee
akothee

Akothee alimwacha Omosh mara baada ya fungate huko Ugiriki, baada ya kugundua baadhi ya mambo kumhusu. Hiyo ilikuwa ni miezi miwili tu baada ya harusi yao iliyotangazwa sana.

 

"Nilitoka nje ya uhusiano mnamo Juni. Kwa kawaida mimi hutoka nje ya mahusiano yangu nikiwa bado ndani yake. Tulipokuwa kwenye fungate, niligundua baadhi ya mambo ambayo sikuweza kustahimili. Kisha akaniuliza, “Je, utaniacha?” Nikasema, “Hapana, mpenzi, nakupenda”. Nilipokuwa nikiondoka Uswizi mwezi Julai, kwenye uwanja wa ndege, aliniuliza, "Je, utaniacha?, Nikasema "Hapana, mpenzi, nakupenda". Lakini kwa hakika, nilikuwa tayari nimeondoka,” alisimulia mwaka jana