Kajala athibitisha binti yake Paula anatarajia kupata mtoto hivi karibuni

Kajala alionesha furaha akifichua taarifa hizo ila akaonesha hisia kwamba bintiye aliharakisha kwani yeye [Kajala] hakuwa tayari kuanza kuitwa nyanya kwani bado yeye ni mbichi na ana damshi.

Muhtasari

• Kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa, Paula na msanii Marioo wamekuwa katika kile kinachotajwa kuwa mapenzi mazito,

Kajala anatarajia kuitwa bibi
Kajala anatarajia kuitwa bibi
Image: Instagram

Muigizaji mkongwe wa Bongo Fleva, Kajala Masanja Fridah amethibitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram kwamba hivi karibuni ataitwa bibi [nyanya] shukrani kwa juhudi za haraka za bintiye wa kipekee, Paula Kajala.

Kajala alionesha furaha akifichua taarifa hizo ila akaonesha hisia kwamba bintiye aliharakisha kwani yeye [Kajala] hakuwa tayari kuanza kuitwa nyanya kwani bado anajiona mbichi licha ya umri wake kusonga kwa kasi ya ajabu.

“Ila Paula muda wa kuwa bibi ulikuwa bado kidogo jamani,” Kajala aliandika akiwa katika picha nzuri kwenye ufuo wa bahari.

Kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa, Paula na msanii Marioo wamekuwa katika kile kinachotajwa kuwa mapenzi mazito, huku Kajala mwenyewe akiliafiki penzi lao na kumtaja waziwazi Marioo kama mkaza mwana wake.

Mwaka jana, Paula na mamake Kajala walithibitisha kwamba Marioo alikuwa amewasilisha mahari za Zaidi ya milioni 100 za kitanzania kwa ajili ya kumuoa kabisa mrembo huyo ambaye pia ni mjasiriamali wa mavazi.

“Tayari ametoa mahari milioni 100,” Paula alijibu swali hilo huku wakicheka na mama yake na kujaribu kuficha nyuso.

Licha ya udogo wa umri wake, binti huyo amekuwa katika mzunguko wa kimapenzi hapo awali na msanii Rayvanny ambaye mapema mwaka jana waliachana baada ya Rayvanny kumrudia mpenzi wake wa zamani, Fahyma.