Esma Platnumz aorodhesha sababu kuu 5 kwa nini hawezi muacha mpenzi wake mpya

“Simuachi kwa kufikiria ndugu wataniona aje au marafiki. Ninachojali mimi ni furaha yangu. Pia simuachi eti kisa hana hela, tutatafuta wote tutaleta mezani,” aliongeza.

Muhtasari

• Esma alisema kwa umri aliokuwa nao, hawezi kuchukuliwa na maamuzi kisa ndugu watamuchukulia kivipi.

Esma Platnumz, dadake msanii anayetajwa kama mtumbuizaji bora wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amezama kwenye penzi lake jipya na mwanamume anayefahamika kwa jina Jembe One.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Esma Platnumz ameachia orodha ndefu ya sababu kuu tano ni kwa nini hawezi kushawishika kumuacha mpenzi wake mpya ambaye wanatarajia kufunga harusi hivi karibuni.

Kwa mujibu wa maelezo yake, mjasiriamali huyo hayuko tayari kumuacha mpenziwe kwa kuambiwa kwamba yuko na mwanamke mwingine au ana watoto wengine nje ya uhusiano.

“Simuachi mume wangu eti kisa kuna mtu kasema kachepuka naye, simuachi eti kisa kazaa nje, mtajuana wenyewe mnavyolea mtoto wenu kwa kujiiba iba,” Esma alisema kwa ukakamavu wa kipekee.

Esma alisema kwa umri aliokuwa nao, hawezi kuchukuliwa na maamuzi kisa ndugu watamuchukulia kivipi bali anachokiangalia Zaidi ni furaha ya nafsi yake, hivyo kusema kwamba hayuko tayari kusikiliza be wala tu kutoka kwa familia, ndugu, jamaa wala marafiki kumhusu Jembe One.

“Simuachi kwa kufikiria ndugu wataniona aje au marafiki. Ninachojali mimi ni furaha yangu. Pia simuachi eti kisa hana hela, tutatafuta wote tutaleta mezani,” aliongeza.

Alimaliza kwa kuwashauri wanawake wenza kwamba huku nje ni kugumu na ni afadhali watulie na yule mwanamume waliye naye ambaye wanahadaiwa kuwa ni mbaya kumbe huku nje anaonwa kama almasi ya warembo.

“Simuachi eti kisa kachafua hali ya hewa kwa dada Mange au kwa Maimatha. Nje kugumu, mtulie na waume wenu, uliyempata huyo ndiye Mungu kakupa ridhiki yako sasa wewe hangaika watu wengi nje wanaungua,” Esma alimaliza kwa ushauri.