Diamond apata wakati mgumu kuchagua kati ya vixen wa Mapoz na mpenziwe Zuchu

Akitetea uamuzi wake wa kumpenda Zuchu pekee, Diamond alithibitisha kwamba kwa sasa msanii huyo si mchumba bali ni mke wake kabisa kwani ameshamuweka ndani.

Muhtasari

• Walikuwa wamechukua picha hizo katika mionekano na mapozi tofauti huku mkononi wakiwa wameshika mpira wa vikapu wakijivinjari kama wapenzi.

Image: Instagram

Msanii Diamond Platnumz baada ya kuachia video yake ya ngoma ya Mapoz siku mbili zilizopita, Alhamisi aliachia mfululizo wa picha kutoka kwa maandalizi ya video hiyo jinsi yalivyokuwa.

Katika mfululizo wa picha hizo, alishiriki picha ambazo walikuwa wanaigiza na vixen wake kama wachumba huku wakiwa wamevaa jezi za mpira wa vikapu za timu ya Lakers kutoka Marekani.

Walikuwa wamechukua picha hizo katika mionekano na mapozi tofauti huku mkononi wakiwa wameshika mpira wa vikapu wakijivinjari kama wapenzi.

Kwa muonekano huo wenye ukakasi, mashabiki walianza kumburura Diamond baadhi wakihisi kwamba kulikuwa na kitu Zaidi tu ya kazi ya kwenye video.

Mmoja kkatika mtandao wa Instagram alimuuliza kufanya chaguo kati ya vixen huyo kwenye video yake ya Mapoz na msanii wake Zuchu ambaye anamtaja kama mpenzi wake kwa Zaidi ya miaka miwili sasa.

Jibu la Diamond liliwaacha wengi vinywa wazi, kwani alisema kwamba licha ya kuonekana kuendana kwa kiasi kikubwa na vixen huyo, bado moyo wake upo kwa Zuchu pika-pakua.

Akitetea uamuzi wake wa kumpenda Zuchu pekee, Diamond alithibitisha kwamba kwa sasa msanii huyo si mchumba bali ni mke wake kabisa kwani ameshamuweka ndani.

“Zuchu [ndio mzuri] ndio maana yuko ndani,” Diamond alijibu.

Licha ya kudaiwa kuwa wapenzi kwa Zaidi ya miaka 2, Diamond na Zuchu hawajafanikiwa kuwa na mtoto pamoja, kinyume na jinsi msanii huyo alikuwa akipata mtoto kwa haraka na wapenzi wake wa awali, akiwemo Hamisa Mobetto, Zari Hassan na Tanasha Donna.