Kelechi Africana adai Zuchu kaiba melody ya ngoma yake... kumbe wote wame'copy Mjamaika

Lakini kwa kusikiliza ngoma ya Kelechi Africana 'Alcoholic' na ile ya Zuchu 'Zawadi' tulibaini kwamba wasanii hao wote waliiga melody ya wimbo wa Reggae wa Sophia George ' Girlie girlie' wa mwaka 1985.

Muhtasari

• Wimbo wa Zuchu kuanzia sekunde ya 41, wa Kelechi kuanzia sekunde ya 51 na wimbo original wa Sophia George kuanzia sekunde ya ya 13.

ZUCHU NA KELECHI AFRICANA
ZUCHU NA KELECHI AFRICANA
Image: FaCEBOOK

Kwa mara nyingine Sanaa ya muziki baina ya Kenya na Tanzania imetumbukia katika mzozo wa vita baridi baada ya msanii wa Kenya Kelechi Africana kutoka Pwani kumtuhumu mwenzake Zuchu kutoka Tanzania kwa dai kwamba ameiba melody ya wimbo wake.

Kelechi kupitia kurasa zake katika mitandao ya kijamii aliweka uthibitisho huo akisema kwamba wimbo mpya wa Zuchu ‘Zawadi’ ambao umetoka siku chache zilizopita kwa asilimia kubwa katika upande wa melody umeiga wimbo wake [Kelechi] kwa jina ‘Alcoholic’ ambao alitoa Zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

“Zuchu aotea ngoma yangu,” Kelechi Africana aliandika kwenye screenshot ya wimbo wake wa Alcoholic akirekodi melody ya wimbo huo.

Ila kwa kuzama Zaidi, Radiojambo.co.ke katika upekee wetu tuliweza kubaini kwamba ni kweli melody zote zinafanana kwa ukaribu lakini pia wasanii wote tunaweza tukasema walifanya sampling ya melody original kutoka kwa msanii wa kike mkongwe kutoka Jamaika, Sophia Goerge.

Sophia George katika wimbo wake maarufu uliompa umaarufu duniani mwaka wa 1985 – Girlie Girlie – ndiko wanakokisiwa kutoa melody hiyo ambayo sasa hivi wawili hao wanazozania, Kelechi akisema kwamba meody ni ya kwake ambayo Zuchu ameotea.

Hebu sikiliza ngoma hizi zao na kisha ukaisikilize ya Mjamaika kama unaweza kubaini hilo;

Wimbo wa Zuchu kuanzia sekunde ya 41, wa Kelechi kuanzia sekunde ya 51 na wimbo original wa Sophia George kuanzia sekunde ya ya 13.