"Lakini mko na njaa" Betty Kyallo asema makumi ya wanaume wakifurika kwenye DM yake

“Lakini mko na njaa, DM yangu imeshika moto leo, nyinyi wote tulieni, sikumaanisha kwamba natafuta mtoto wala kutaka…" alisema.

Muhtasari

• “Lakini mko na njaa, DM yangu imeshika moto leo, nyinyi wote tulieni, sikumaanisha kwamba natafuta mtoto wala kutaka…" alisema.

Betty Kyallo.
Betty Kyallo.
Image: Instagram

Mtangazaji wa runingani Betty Kyallo amezua mjadala mkali miongoni mwa wanaume baada ya kupakia picha yake akiwa katika hali ya kuonesha urembo wake uliopitiliza.

Siku ya Ijumaa, Kyallo aliwaacha wanaume wakimtolea macho ya kumtamani kimapenzi baada ya kuachia picha hiyo akiwa amevalia vazi la waride.

Msichana huyo wa zamani wa runinga, bintiye na mama yake waliondoka hadi Mombasa ili kutumia wakati mzuri pamoja baada ya sherehe ya siku ya wapendanao.

Katika picha hiyo mahususi, Betty alikuwa ameketi chini, hatua chache kutoka kwenye kidimbwi cha kuogelea.

Baada ya wanaume wengi kujitoa wazimu katika upande wa kutolea maoni, mama huyo wa binti mmoja alikwenda kwenye Insta stories zake na kusema anafikiria kuongeza binti mwingine katika maisha yake.

“Nina mtoto mmoja, najaribu kutengeneza nafasi ya mwingine,” aliandika.

Bila kujua kwamba hii ilikuwa fursa ya kuwafungulia wanaume nafasi kujaza DM yake kila mmoja akijipigia debe kwamba ana uwezo wa kumpa binti mwingine huku wengine wakitaka awaasili kama watoto wake.

Lakini akiwajibu, Kyallo alisema kwamba ni njaa inawasumbua huku akisema kwamba kwa kusema anajaribu kutengeneza nafasi ya mtoto mwingine hakuwa na maana kwamba anatafuta au anataka ku’adopt.

“Lakini mko na njaa, DM yangu imeshika moto leo, nyinyi wote tulieni, sikumaanisha kwamba natafuta mtoto wala kutaka… na pia hapana, siwezi kumuasili kijana wa miaka 23 wa kiume kama mtoto wangu. Samahani jamani nieleweni,” alisema.

kyallo
kyallo