Muigizaji Wolper aapa kuzaa hadi watoto 6 ili kuwakomesha waliomdhihaki kuwa ni tasa

“Yaani mna haki kuniambia nina mimba jamani, eeh… kitambi kimeongezeka balaa, lakini sina mimba, sina! Washenzi wakubwa nyie." alisema.

Muhtasari

• “Nina stress zangu tu yaani hapa ni kula na kusimamia mambo yangu, sina mimba." alisema.

Jackline Wolper na wanawe
Jackline Wolper na wanawe
Image: Instagram

Muigizaji mkongwe wa filamu za Bongo ambaye pia ni mjasiriamali Jackline Wolper ameweka wazi kwamba kwa sasa hana mimba nyingine baada ya watu kuanza kushuku ukubwa wa tumbo lake.

Mama huyo wa watoto wawili alisema japo kwa sasa hana mimba, lakini hata akipata mimba ataificha hadi watu waje kushutkia siku ya mwisho kuwa ana mtoto, kama ambavyo amefanya awali kwa watoto wake wawili.

“Yaani mna haki kuniambia nina mimba jamani, eeh… kitambi kimeongezeka balaa, lakini sina mimba, sina! Washenzi wakubwa nyie. Na nikiwa nayo naficha vile vile kama kawaida. Uchawi tu ‘una mimba una mimba’” alisema huku akilipiga makofi tumbo lake.

Wolper alifichua kwamba anataka kuja kuwakomesha wote waliomdhihaki kuwa yeye ni tasa ambaye hawezi kubeba ujauzito, akisema kwamba kama njia moja ya kuwakomesha na kuwaziba midomo, atahakikisha amezaa hadi watoto sita.

“Nina stress zangu tu yaani hapa ni kula na kusimamia mambo yangu, sina mimba. Japokuwa ninataka nikimalizana na mambo yangu nizae kweli kweli. Si mliniita mgumba nyine, nitawapa shoo bado, napia hadi sita ndio napumzika,” aliongeza.

Mama P, kama anavyojiita alifunga harusi miaka miwili iliyopita na mpenzi wake Rich Mitindo na wamekuwa wakiyaweka maisha yao ya ndoa mbali na mitandao ya kijamii.