Paula hajulikani kazi yake ni gani, ila tu kutrend kwa sababu ya wanaume – Abby Chams

“Kwa sababu mimi sioni umuhimu wa kuongelea watu ambao hata hatujui kazi zao ni nini, ila tu kutrend kwa sababu ya ku’date wanaume,” Abby Chams alisema.

Muhtasari

• “Simjui mimi, na hiyo picha mnasema tulionekana pamoja labda watu tu walihariri, mimi simjui huyo,” Paula alikataa kata kata kipindi hicho.

Abby Chams na Paula Kajala
Abby Chams na Paula Kajala
Image: Instagram

Ugomvi na malumbano baina ya msanii Abby Chams na aliyekuwa rafiki yake, Paula Kajala unazidi kutokota kwa mieizi kadhaa sasa baada ya Chams kuuibua upya akisema kwamba hana lolote la kumzungumzia binti huyo wa muigizaji Kajala.

Kupitia insta stoty yake, Abby Chams alikuwa akijibu swali aliloulizwa kuhusu bifu lake na Paula Kajala lakini alichokisema kilibaki kuwa mwiba mchungu katika kisigino cha Paula.

Kwa mujibu wa Chams, mtu kama Paula hana nafasi yoyote ya kuzungumziwa kwa mazuri katika jamii kwa kile alisema kwamba binti huyo licha ya kuwa maarufu katika mtandao wa Instagram, bado mashabiki wake wengi hawajui kazi yake maalum inayomuingizia kipato na riziki.

Msanii Chams alizidi kusema kwamba haoni kabisa umuhimu wa kumzungumzia Paula kwani kazi yake kuu ni kugonga vichwa vya habari kwa sababu ya wanaume tu, na hakuna kingine.

“Kwa sababu mimi sioni umuhimu wa kuongelea watu ambao hata hatujui kazi zao ni nini, ila tu kutrend kwa sababu ya ku’date wanaume,” Abby Chams alisema na kumalizia kwa kichezo cha bezo.

Itakumbukwa wawili hao walianza kuzozana mwaka jana pale Chams alipoanya kolabo na Marioo lakini baadae Marioo akaiondoa vesi yake katika wimbo wake na ikasemekana kuwa chanzo kilikuwa Paula – ambaye anachumbiana na msanii huyo.

Baadae Paula alipoulizwa kuhusu Abby Chams, alikanusha wazi wazi kutomjua kabisa licha ya kuwa walikuwa marafiki wa kushibana kipindi cha kabla ya zogo hilo.

Akiulizwa na mwanahabari, Paula kwa kutikisa kichwa alikanusha kabisa kumjua Abby Chams na wala hajawahi kumuona hata kidogo.

“Simjui mimi, na hiyo picha mnasema tulionekana pamoja labda watu tu walihariri, mimi simjui huyo,” Paula alikataa kata kata kipindi hicho.