Jinsi Jackie Matubia alivyokwepa swali kuhusu kusaidiana na Blessing Lung'aho kulea mtoto

Itakumbukwa mwaka jana, Matubia alishiriki video kwenye chaneli yake ya YouTube akiwa na hisia nzito ambapo alisema kwamba haijawa rahisi kwake kama mama kwa binti wawili bila msaada wowote.

Muhtasari

• Licha ya muda mrefu ambao umepita tangu kuzaliwa kwa Zendaya, Matubia alikataa swali hilo kwa busara, akijibu kwa kifupi; "Swali lingine?"

MUIGIZAJI
JACKIE MATUBIA// MUIGIZAJI
Image: FACEBOOK//JACKIE MATUBIA

Muigizaji Jackie Matubia bado anaokenaka kutokuwa tayari kuzungumzia kwa undani suala la kushirikiana katika malezi ya mwanawe pamoja na aliyekuwa mpenzi wake Blessing Lung’aho.

Haya yalithihirika wakati alipoulizwa swali kuhusu hatua walizozipiga na Lung’aho katika suala zima la kumlea binti Zendaya waliyempata pamoja yapata miaka miwili iliyopita.

Kwa ujanja, Matubia alikwepa swali hilo na kumtaka mwanabogu Nicholas Kioko kuendelea kwa swali lingine, kwani hakuwa tayari kabisa kuzungumzia hilo.

“Ni takribani miaka miwili tangu upate mtoto wako wa pili na Blessing Lung’aho na kwa wakati Fulani mkaja mkaachana, kwa hiyo bado mnaendelea kushirikiana kwa ajili ya malezi ya mtoto ama?” Kioko aliuliza.

Licha ya muda mrefu ambao umepita tangu kuzaliwa kwa Zendaya, Matubia alikataa swali hilo kwa busara, akijibu kwa kifupi;

 "Swali lingine?"

Itakumbukwa mwaka jana, Matubia alishiriki video kwenye chaneli yake ya YouTube akiwa na hisia nzito ambapo alisema kwamba haijawa rahisi kwake kama mama kwa binti wawili bila msaada wowote.

Katika video hiyo, alisema kwamba ni Mungu tu amekuwa akimshikilia yeye na binti zake, akiashiria kwamba Lung’aho tangu kuondoka kwake katika maisha yake kimya kimya, alikatisha msaada wake wa malezi kwa bintiye.

“Mungu kwa kweli amekuwa katika kitovu cha maisha yetu, mimi na mabinti zangu, amenishikilia sana wakati kila kitu katika maisha yangu kilikuwa kinasambaratika. Mungu alinishika mkono na kunipa hakikisho kwamba yeye ni Alfa na Omega. Amekuwa baba kwa wanangu na amekuwa nguzo ya kuegemea,” Matubia alisema.

“Umekuwa ni wakati mgumu sana, miezi kadhaa iliyopita nimepitia moto na kusema ukweli nimeona mkono wa Mungu,” aliongeza.

Baadae katika msururu wa video kwenye chaneli hiyo yake, mama huyo wa mabinti wawili alimtupia kijembe Lung’aho aliwashauri kina dada wakati wanataka kuchumbiana, wachague mwanamume mwenye akili.