Mwimbaji Spice Diana kutoka Uganda akiri kulipa wanablogu kusukuma maslahi yake mtandaoni

Diana alijitetea akisema "muziki ni biashara tunapaswa kuwekeza", hii ni baada ya wakosoaji wake kudai kwamba anawalipa wanablogu ili kumtusi kwenye majukwaa yao kupata umaarufu.

Muhtasari

• “Ninapoenda kwenye Jah-Live, lazima nilipe mamilioni kutengeneza wimbo. Ninapoenda Swangz, lazima nilipe mamilioni ili kutengeneza video nzuri,” alisema.

• “Unawezaje basi kumfanya mtu kusukuma unachofanya kwenye jukwaa lake na hutaki kumlipa?”

SPICE DIANA
SPICE DIANA
Image: Instagram

Mwimbaji wa Uganda, Spice Diana amethibitisha kulipa pesa kwa wanahabari, wengi wao wakiwa wanablogu ili kusukuma maslahi yake mtandaoni.

Katika moja ya kipindi cha runinga ya Baba TV Uganda siku chache zilizopita, Mwimbaji huyo alitetea zoea hili, akisema ni mojawapo ya njia chache ambazo wanamuziki wote wa kisasa wanaweza kusukuma muziki wao kwa umma.

"Muziki ni biashara ambayo tunapaswa kuwekeza," alisema.

“Ninapoenda kwenye Jah-Live, lazima nilipe mamilioni kutengeneza wimbo. Ninapoenda Swangz, lazima nilipe mamilioni ili kutengeneza video nzuri,” alisema.

“Unawezaje basi kumfanya mtu kusukuma unachofanya kwenye jukwaa lake na hutaki kumlipa?”

"Mwanamuziki yeyote lazima atafute kile anachouza…watu wanaokosoa kuwekeza kwenye muziki labda hawako kwenye muziki au wanaugua kichwa."

Diana zaidi aliwashauri wakosoaji wake kujifunza kutoka kwake na kupata waandishi wa habari upande wao.

Diana alishambuliwa wiki jana kutoka kwa wakosoaji wa muziki nchini humo wakidai kwamba msanii huyu amekuwa ‘akiwanunua’ wanablogu ili kuangazia habari zake kila mara.

Kando na hilo, mkosoaji mmoja pia alidai kwamba Spice Diana alikuwa anawachagua wanablogu ambao anawalipa ili kumtusi kwenye majukwaa yao, kumbe ni njia moja ya kutafuta umaarufu.