Mbosso ampa burunguti la hela mwanafunzi aliyechapwa shuleni kwa kuandika nyimbo zake (video)

Baada ya simulizi hilo la muda mfupi, Mbosso aliinama kwenye gari na kuhesabu bunda la noti kabla ya kumkabidhi kijana yule kama zawadi ya kuuthamini ushabiki wake kwa kazi zake za sanaa.

Muhtasari

• Alimtaka dereva wake kushusha kioo cha upande wake kabla ya kumuita kijana yule na kufanya gumzo fupi naye.

Mbosso
Mbosso
Image: Screegrab

Msanii Mbosso kutokea WCB Wasafi amekonga nyonyo za mashabiki wake wengi baada ya kukutana na mvulana shabiki yake ambaye alimhadithia kuchapwa shuleni kisa kuandika mistari ya nyimbo zake.

Mbosso ambaye alikuwa akielekea nyumbani ndani ya gari na dereva wake alimuona kijana huyo ambaye waliwahi kutana awali na kumhadithia hivyo.

Alimtaka dereva wake kushusha kioo cha upande wake kabla ya kumuita kijana yule na kufanya gumzo fupi naye.

Kijana yule alisimulia jinsi anavyomkubali Mbosso kiasi kwamba vitabu vyake vingi shuleni alikuwa anaviandika majina na nyimbo za Mbosso shuleni.

"Huyu jamaa nishawahi kutana naye, shabiki wangu sana huyu. Na kuna siku, sehemu hii hii tu aliniambia duh tutakutana tena bana. Mwenyezi Mungu ni mkubwa sana, leo nimemuona tena anapita hapa, njia ile ile, yuko na rafiki zake leo. Huyu hapa shabiki wangu, nishushie kioo," Mbosso alisikika akimueleza dereva wake.

Mbosso alimuita kijana huyo ambaye alijongea upande wa dirisha lake kwenye gari na kuanza kumsimulia jinsi yalimtokea makubwa shuleni baada ya kupatikana ameandika nyimbo za Mbosso kwenye daftari.

"Nimefurahi sana, mwanangu halafu nakuota kinoma yaani, sema kuna daftari nilikuwa naandika Mbosso, ilikuwa naimba hivi mwisho wa siku daftari lenyewe hisabati nikaandika Mbosso Diamond likafika kwa mwalimu akanipiga bakora," kijana huyo alieleza.

Baada ya simulizi hilo la muda mfupi, Mbosso aliinama kwenye gari na kuhesabu bunda la noti kabla ya kumkabidhi kijana yule kama zawadi ya kuuthamini ushabiki wake kwa kazi zake za sanaa.

Tazama video ya tukio zima hapa;