Diana amjibu Bahati kuwa anampenda akiwa na nywele kila sehemu baada ya kumlalamikia

“Inakuaje mwanamume aliyeoa, awe na nywele kama hivi?” Bahati aliuliza huku akionyesha kwapa lake kwenye kamera.

Muhtasari

• Licha ya Diana kujitetea, Bahati alisisitiza kwamba suala la usafi wa mwili wake si lake binafsi bali ni la mke wake.

• “Mpenzi wangu kubali kwamba hupendi kujitunza, angalia jinsi ulivyo, angalia nywele. Ungekuwa umejitengeneza ndio ukuje useme,” Diana alimuambia.

Diana na Bahati
Diana na Bahati
Image: Screengrab

Wakuza maudhui wa YouTube, Diana Marua na mumewe wamerejea tena na kipindi chao, safari hii wakitaniana kwa kutupiana lawana.

Bahati alilalamika kwamba mkewe Diana amemtelekeza katika kumfanyia usafi wa kumnyoa nywele katika mwili wake.

Msanii huyo alisema kwamba ana takribani miaka 3 na nywele katika sehemu zote za mwili wake, na mkewe wala hajali, akilalamika kuwa hiyo ni sawa na mkewe kutepetea katika jukumu lake la kuhakikisha mumewe anakaa msafi.

“Inakuaje mwanamume aliyeoa, awe na nywele kama hivi?” Bahati aliuliza huku akionyesha kwapa lake kwenye kamera.

Hata hivyo, Diana alimjibu kwamba anampenda akiwa na nywele zote katika mwili wake, haswa katika sehemu za siri.

“Wacheni niwaambie, mnajua ni mara ngapi ninamuambia Bahati njoo nikunyoe, na mnajua yeye hawezi jinyoa mwenyewe. Yeye heri akae nayo kwa miaka 10, hawezi. Lakini nywele za hapo chini nazipenda jinsi ilivyo hivyo, napenda ukiwa na nywele. Mimi nakaa vile wewe utafurahia, hata mimi nafurahia ukiwa hivyo,” Diana alisema.

Licha ya Diana kujitetea, Bahati alisisitiza kwamba suala la usafi wa mwili wake si lake binafsi bali ni la mke wake.

“Mpenzi wangu kubali kwamba hupendi kujitunza, angalia jinsi ulivyo, angalia nywele. Ungekuwa umejitengeneza ndio ukuje useme,” Diana alimuambia.

Bahati alimaliza akimpa mkewe onyo kwamba mwaka huu anahitaji kujiongeza kidogo katika kumwajibikia.