"Mia, tunakupenda" Zubeidah Kananu amfariji binti wa Rita Tinina wa miaka 8

Zubeida pia alitoa pole kwa binti yake, marafiki na familia kwa niaba ya waandishi wengine wa habari.

Muhtasari
  • Zubeida mwenye hisia kali, alishindwa kuficha machozi yake huku sauti yake iliyokuwa imezidiwa na hisia na majonzi, ikipenya ukimya mzito wa mazishi na kuwatoa watu machozi.

Rais wa Chama cha Wahariri Kenya Kananu Jumatano alitoa heshima ya kihisia kwa marehemu Mwanahabari Rita Tinina.

Zubeida mwenye hisia kali, alishindwa kuficha machozi yake huku sauti yake iliyokuwa imezidiwa na hisia na majonzi, ikipenya ukimya mzito wa mazishi na kuwatoa watu machozi.

Kila neno lilionekana kutetemeka kwa uzito wa huzuni.

"Inauma sanaaa.Rita alikuwa mmoja wetu na tunahuzuni kupugukiwa sana. Inauma sanaa," Zubeida alisema.

Wanafunzi wenzake wa zamani wa Rita kutoka shule ya upili ya  Masaai Girls, la 1995, katika heshima zao walimtaja kama mtu mwenye furaha na upendo na kuongeza kuwa kifo chake kiliacha shimo kubwa mioyoni mwao.

"Msichana kila mara ulipoonekana kwenye skrini zetu, majivuno yalitujaa ulipowakilisha vyema jamii ya Wasichana wa Maasai. Kila tulipokuona jukwaani tulihisi wakilishwa. shujaa ameanguka kweli. Umekimbia mbio zako, umemaliza mbio zako, hakika kuna taji limewekwa kwa ajili yako.”

Mwakilishi wa Maasai Girl katika mazishi yake alisema. Pia walituma salamu zao za rambirambi kwa bintiye Malkia, mshirika Robert Nagila na familia. Mwandishi wa habari wa NTV na mwenyekiti wa kamati ya mazishi ya Tinina Duncan Khaemba aliwashukuru marafiki na familia kwa michango yao ya ukarimu kusaidia bili.

Mwili wa Rita ulisafirishwa hadi nyumbani kwake kwa gari la kukodi la Range Rover kama alivyoahidiwa na marafiki zake.

Watu waliohudhuria mazishi yake ni wanahabari kutoka vituo mbalimbali vya habari.

Zubeida pia alitoa pole kwa binti yake, marafiki na familia kwa niaba ya waandishi wengine wa habari.

“Mia tunakupenda. Mungu na nguvu na tutaendelea kukushika mkono. Kwa niaba ya wahariri wote, tunatoa pole zetu. Mungu atupe nguvu na ailaze roho yake pahali pema palipo na wema”

Mama wa mtoto mmoja alipatikana nyumbani kwake Kileleshwa Jumapili Machi 17.

Aliacha binti yake mwenye umri wa miaka 8 Malkiah na mwenzi wake Robert Nagila.