Hatua zilizochukuliwa na chama cha waigizaji Nigeria baada ya muigizaji Junior Pope kufa maji

Pia ilitangaza Alhamisi kuwa siku ya kutofanya filamu yoyote kwa kimombo "No Shoot Day" kwa watengenezaji filamu wote wa Nollywood, kufuatia vifo vya mwigizaji Junior Pope na wahudumu wengine watatu

JUNIOR POPE.
JUNIOR POPE.
Image: Instagram

Chama cha waigizaji wa filamu nchini Nigeria kimetangaza hatua kabambe za kuchukuliwa kuanzai sasa kwenda mbele ili kuzuia vifo vya waigizaji wake.

Hii ni baada ya muigizaji Junior Pope kutangazwa kufariki baada ya boti alimokuwa ndani na wenzake watatu kuzama.

Chama hicho kimetangaza kusimamisha utayarishaji wa filamu zote zinazohusisha maeneo ya mito na kupanda boti kufuatia ajali mbaya ya boti iliyogharimu maisha ya mwigizaji wa Nollywood Junior Pope na wafanyakazi watatu.

Pia ilitangaza Alhamisi kuwa siku ya kutofanya filamu yoyote kwa kimombo "No Shoot Day" kwa watengenezaji filamu wote wa Nollywood, kufuatia vifo vya mwigizaji Junior Pope na wahudumu wengine watatu waliokufa katika ajali ya boti kwenye Mto Anam huko Anambra siku ya Jumatano.

Emeka Rollas, Rais wa Kitaifa wa chama hicho, alisema katika taarifa yake siku ya Alhamisi kwamba ajali hiyo ilitokea kwenye seti ya filamu inayoitwa ‘’The Other Side of Life’’, iliyotayarishwa na Adamma Luke.

"Kufuatia tukio la kusikitisha la ajali ya boti iliyogharimu maisha ya Junior Pope na wahudumu wengine watatu kwenye kando ya maji ya Mto Niger Cable Point Asaba mnamo tarehe 10 Aprili, filamu zote zinazohusisha maeneo ya mito na upandaji boti zinasitishwa kwa muda usiojulikana.”

"Hakuna kufanya filamu katika maeneo yote nchini kote mnamo Alhamisi, 11 Aprili 2024 na filamu inayoitwa "The Other Side of Life’’ imesimamishwa kwa muda usiojulikana.”

 

"Pia, hakuna mwigizaji anayeruhusiwa kufanya kazi na Adamma Luke kama mtayarishaji hadi taarifa zaidi, wakati tunaendelea kutafuta miili ya watu waliobaki.”

"Roho zao zipumzike kwa amani," alimaliza.

Kifo cha Junior Pope kinajiri mwezi mmoja tu baada ya kifo cha muigizaji mwingine kwa jina Mr Ibu.