Sitaki kupata mtoto mwingine kwa angalau miaka 7 ijayo – Vera Sidika

“Vitu vinne ambavyo sitaki vinipate majira ya msimu wa joto ni kupata mimba, kufilisika, kuwa na huzuni na kupata mimba.”

Muhtasari

• Pia huwaonyesha watoto wake wawili warembo; Asia na Ice mtandaoni wakitoa maelezo ya wazi kuzihusu.

• Kwa sasa, Vera anaishi na wanawe bila baba yao, Brown Mauzo kwenye nyumba moja baada ya wawili hao kuweka wazi kuhusu utengano wao mwaka jana.

Vera Sidika
Vera Sidika
Image: FB

Mwanasosholaiti Vera Sidika ametangaza msimamo wake kuhusu mustakabali wa idadi ya watoto anaotarajia kuwapata siku zijazo.

Mama huyo wa watoto wawili kupitia ukurasa wake wa Instagram alionekana kutosheka na idadi ya wanawe kwa sasa huku akisema kwamba hana mpango wa kuongeza mtoto kwa angalau miaka 7 ijayo.

“Hakuna watoto Zaidi kwangu kwa angalau miaka 7 ijayo. Hapana,” Vera Sidika aliandika.

Kwenye ujumbe huo, Sidika aliongeza kwamba msimu ujao wa joto, kuna baadhi ya vitu ambavyo atahakikisha amevikwepa kabisa navyo ni kupata mimba, kuwa na huzuni na kufilisika.

“Vitu vinne ambavyo sitaki vinipate majira ya msimu wa joto ni kupata mimba, kufilisika, kuwa na huzuni na kupata mimba.”

Awali, mjasiriamali huyo wa huduma za urembo aliweka wazi kwamba anatafuta mtu mwenye uwezo wa kumtoboa masikio yake, akisema kuwa anataka kuongeza matobo 5 zaidi.

"Ninahitaji kutoboa masikio matobo 5 zaidi. Nani bora zaidi jijini Nairobi…Kwa simu za Nyumbani leo,” alishiriki matamanio yake kwenye Instastories zake.

Vera Sidika anajulikana sana kwa mtindo wake wa maisha ya kifahari, mara nyingi akienda kwenye mitandao ya kijamii ili kuwapa wafuasi wake mwonekano wa maisha yake.

Pia huwaonyesha watoto wake wawili warembo; Asia na Ice mtandaoni wakitoa maelezo ya wazi kuzihusu.

Kwa sasa, Vera anaishi na wanawe bila baba yao, Brown Mauzo kwenye nyumba moja baada ya wawili hao kuweka wazi kuhusu utengano wao mwaka jana.