Burna Boy aeleza sababu za kutofikiria kupata watoto kwa sasa, "mama ananipenda sana!" (video)

Burna Boy alisema kwamba kwa sasa hawezi kujiondoa katika mapenzi ya wazazi wake na kuanza safari ya kutafuta mtoto wake mwenyewe, akifichua kwamba mamake na babake wanampenda kupindukia.

Muhtasari

• Kulingana naye, anataka kuwa na uwezo wa kuwapa watoto wake upendo na uangalifu zaidi kuliko yale aliyopokea kutoka kwa wazazi wake.

Burna Boy
Burna Boy
Image: Facebook

Mwimbaji maarufu wa Nigeria, Burna Boy, amefunguka kuhusu sababu zinazomfanya bado kutofikiria kupata mtoto wa kwake wa kumzaa licha ya umri kwenda na kuwa na ufanisi mkubwa kutokana na muziki wake.

Katika video, msanii huyo aliyeshinda tuzo alifafanua kuwa hana mtoto kwa sababu hayuko tayari kuwa baba wa yeyote bado.

Kulingana naye, anataka kuwa na uwezo wa kuwapa watoto wake upendo na uangalifu zaidi kuliko yale aliyopokea kutoka kwa wazazi wake.

Alizidi kukwepa uvumi wote uliokuwa ukienea kuwa hana uwezo wa kuzaa mtoto.

Katika video hiyo, Burna Boy alisema kwamba kwa sasa hawezi kujiondoa katika mapenzi ya wazazi wake na kuanza safari ya kutafuta mtoto wake mwenyewe, akifichua kwamba mamake na babake wanampenda kupindukia.

Kwa maneno yake:

"Sitaki kuwa na watoto bado. Umeona operesheni yangu kaka? Umemuona mama yangu jinsi anavyonipenda? Umemuona baba yangu jinsi anavyonipenda? Najua siwezi kumpa mtu yeyote hivi sasa na maisha ninayoishi.”

"Unanihisi hivyo... ninapotulia na ninahisi ninaweza kuwa kwa ajili ya watoto wangu kila siku na kila dakika sina mtoto. Ninahisi kama watoto wangu wanastahili bora kuliko nilivyopata. Wacha tuseme sikuweza kupata watoto, kuna kama IVF ambayo naweza kufanya kuwa nayo. Kwa hivyo uvumi huo sio kweli."

Tazama video hapa chini: