Rightone aeleza kwa nini alienda nyumbani kwa Dem wa Facebook

Ile siku ataokoka ninaeza fikiria hiyo story kwa sababu saa hii ako na dhambi nyingi sana.”

Muhtasari

•Ile siku ataokoka ninaeza fikiria hiyo story kwa sababu saa hii ako na dhambi nyingi sana.”

•Dem Wa Facebook ananiambia, chairman mimi nitakatalia kwako ananiambia kabisa nakupenda yaani yeye ndio ameniambia ananipenda kabisaa!

Ringtone.
Ringtone.
Image: Instagram

Msanii wa nyimbo za injili Ringtone Apoko ameeleza kwa nini alitembelea Dem wa facebook huko Kayole.

Akizungumza na waandishi wa habari, msanii huyo wa nyimbo za Injili alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu Dem Wa Facebook alionyesha kumtaka kitu ambacho hakuna aliyewahi kumfanyia.

“Dem Wa Facebook ananiambia, chairman mimi nitakatalia kwako ananiambia kabisa nakupenda yaani yeye ndio ameniambia ananipenda kabisaa!!.” Ringtone aeleza.

Hii ni baada ya Ringtone Apoko kuonekana ndani ya nyumba ya Dem Wa Facebook.

Mwimbaji huyo alisema kuwa katika utafiti wake wa kutafuta mpenzi mzuri, alimtawaza Dem Wa Facebook kama aina bora ya mwanamke ambaye angependa kuishi naye kwa sababu ya jinsi alivyo mchapakazi, amedhamiria na ni mstahimilivu.

“Kama unataka kuoa,nimefika mahali nikaona mtu ambaye anakaa raw material ya kuolewa napenda wasichana wako na kimbelembele ya kuwork hard sipendi watu wavivu kwa kitu kile wanafanya. Sababu ambayo napenda Dem Wa Facebook anajituma sana na ako na kimbelembele ya kujituma.” Ringtone alieleza.

Ringtone pia alieleza kuwa yeye ndiye anayelingana kikamilifu na Dame Wa Facebook kwa sababu, tofauti na Obinna, hana watoto kama Dem wa Facebook. Alikubali, hata hivyo, kwamba anaweza kufikiria tu kuchukua Dem Wa Facebook wakati atakuwa amebadilisha njia zake na kuwa mcha Mungu.

“Ile siku ataokoka ninaeza fikiria hiyo story kwa sababu saa hii ako na dhambi nyingi sana.” Ringtone alisema.