Eddie Butita amshukuru rais Ruto kwa kumpa ‘connection’ ya kukutana na Steve Harvey

“"Nilikuona kwenye Youtube" maneno kutoka kwa Steve Harvey. Asante Mheshimiwa Rais kwa ‘connection’ hii ya heshima, kukutana na Steve Harvey Imekuwa ndoto kwa miaka 14 iliyopita leo imetimia,” Butita alisema.

Muhtasari

• Butita pia alifafanua kiini cha mazungumzo yao na Harvey pindi baada ya kukutana, na kusema kwamba Harvey jambo la kwanza alimwambia ni kwamba ‘nilikuona kwenye YouTube’.

Eddie Butita akutanishwa na Steve Harvey.
Eddie Butita akutanishwa na Steve Harvey.
Image: Instagram

Mkurugenzi mtendaji wa blogu wa SPM Buzz, Eddie Butita amemshukuru rais William Ruto kwa kumuunganisha na mtangazaji maarufu wa vipindi vya runingani kutoka Marekani, Steve Harvey.

Butita ambaye ni miongoni kwa kundi kubwa la Wakenya walioandamana na rais katika ziara ya kiserikali ya siku 4 nchini Marekani walikutana na Harvey katika jimbo la Atlanta, Gerogia baada ya ziara katika studio maarufu ya Tyler Perry.

Akichukua kwenye Instagram, Butita alishukuru rais Ruto kwa nafasi hiyo adimu ya kumkutanisha na Harvey ambaye alimtaja kama mtu ambaye amekuwa akitamani kukutana naye katika kipindi cha miaka 14 iliyopita.

Butita pia alifafanua kiini cha mazungumzo yao na Harvey pindi baada ya kukutana, na kusema kwamba Harvey jambo la kwanza alimwambia ni kwamba ‘nilikuona kwenye YouTube’.

“"Nilikuona kwenye Youtube" maneno kutoka kwa Steve Harvey. Asante Mheshimiwa Rais kwa ‘connection’ hii ya heshima, kukutana na Steve Harvey Imekuwa ndoto kwa miaka 14 iliyopita leo imetimia,” Butita alisema.

Muongozaji huyo wa vipindi vya ucheshi alisema kuwa waliweza kufanya mazungumzo ya maana na Harvey kuhusu jinsi ya kuwakimu vijana kwenye tasnia ya biashara na showbiz.

“Tulikuwa na mazungumzo mazuri kuhusu jinsi ya kuandaa na kutoa mafunzo kwa vipaji kwa ajili ya mafanikio ya biashara katika showbiz ni maonyesho na Biashara na nina furaha kuwa wabunifu wetu wamehusishwa katika mazungumzo haya,” Butita alisema.

Jumapili, Butita alifichua kwamba alikuwa na furaha kutajwa miongoni mwa Wakenya ambao walikuwa wameratibiwa kuongozana na rais katika mwaliko rasmi wa ikulu ya White House na rais Joe Biden.

Baada ya kutua katika jimbo la Atlanta Georgia siku mbili zilizopita, Jumatano rais na kundi lake wanatarajiwa kusafiri hadi jimbo la Washington DC ambako wanatarajiwa kushiriki chakula cha jioni kwenye ikulu ya White House baadae kabla ya kufanya mzungumzo na rais Biden.