Kanze Dena asimulia kulewa baada ya kushawishiwa na rafiki

"Nilikunywa pilsner ya kwanza, ya pili, tatu. Tukajipata tumemaliza create mzima. Lakini sinywi tena.”

Muhtasari

•Aliyekuwa msemaji wa Ikulu, Kanze Dena alifunguka kuhusu maisha yake ya zamani, na kufichua kuwa hanywi tena pombe.

•Kanze alisimulia jinsi rafiki yake alivyomshawishi kwenda kwenye kilabu baada ya kazi na akaishia kulewa na kukaa muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa.

KANZE DENA
Image: HISANI

Aliyekuwa msemaji wa Ikulu Kanze Dena alisimulia jinsi rafiki yake alivyomshawishi kwenda kwenye club baada ya kazi na akaishia kulewa.

Kanze Dena alishiriki mahojiano kuhusu maisha yake ya zamani, akifichua kuwa alikuwa akinywa pombe baada ya ushawishi kutoka kwa rafiki yake.

Akizungumza katika mahojiano alipoulizwa kuhusu ushauri mbaya zaidi aliowahi kupokea, alifunguka kuhusu tukio la zamani.

Kanze alifichua kuwa baada ya kumaliza shule ya upili, alianza kufanya kazi kama mhudumu katika mkahawa mmoja jijini Nairobi.

Alisema siku moja baada ya kutoka kazini, kulikuwa na msongamano mkubwa wa magari. Rafiki yake alimwomba atulie kwenye kilabu  ili kusubiri trafiki ipungue, na akaishia kunywa zaidi ya kutosha.

"Nilikunywa pilsner ya kwanza, ya pili, tatu. Tukajipata tumemaliza create mzima. Lakini sinywi tena.”

Kanze alisema aliipenda pombe hiyo kwa sababu ya tangazo lake maarufu la kwenye televisheni, lakini tangu wakati huo ameokolewa.

 

 "Mungu alinikomboa. Asante Yesu," alisema.