Nameless aeleza jinsi anavyowafundisha watoto wake kukabiliana na chuki za mtandaoni

"Bila shaka akaunti zao zote ziko kwa simu yangu na simu ya mamake, kwa hiyo tunaona chochote kinachotokea," alisema.

Muhtasari

•ameless alifunguka na kusema kuwa anawalinda sana watoto wake na anachagua wanachopaswa kuona na kile ambacho hawapaswi kukiona kwa njia halali

•Alisema amewafanya watoto wake kuelewa kuwa baba yao ni mashuhuri, na hilo linakuja na changamoto nyingi.

Nameless na Wahu
Nameless na Wahu
Image: Facebook

Mwanamuziki mkongwe wa Kenya Nameless amefichua jinsi anavyowafunza watoto wake kukabiliana na unyanyasaji wa mtandaoni.

Akiongea katika mahojiano, Nameless alifunguka na kusema kuwa anawalinda sana watoto wake na anachagua wanachopaswa kuona na kile ambacho hawapaswi kukiona kwa njia halali.

"Hata kwangu, kwa familia yangu, ninalinda sana, hata kwa watoto wetu. Ni kama sisi ni watu mashuhuri. Tunafanya mafunzo mengi na watoto wetu.

Lazima niendelee kuwaambia na kuelewa mambo kama chuki na kwamba sio kila mtu anakutakia mema, hata wakati mimi sipo. Wanaelewa maisha hayo." Nameless alisema.

Aliendelea kusema kuwa amewafanya watoto wake kuelewa kuwa baba yao ni mtu mashuhuri, na hilo linakuja na changamoto nyingi kwani wapo ambao wanaweza kuwa wanamchukia.

Hata hivyo, anasema anadhibiti akaunti za mitandao ya kijamii za watoto wake na ana uwezo wa kuchuja taarifa wanazoweza kuziona na kuepuka taarifa mbaya au watu binafsi wanaojaribu kuwakashifu.

“Bila shaka akaunti zao zote ziko kwa simu yangu na simu ya mamake, kwa hiyo tunaona chochote kinachotokea, na kutumia simu ananiuliza, na haya yote tulimjulisha na tunamwambia kwamba hayo tunaofanya ni kwa manufaa yao. Sisi ni kama makocha wako.” Nameless aliongezea.

Nameless anaamini kwamba wazazi ndio wakufunzi wa watoto wao, na wanawajibika kikamilifu kwa jinsi watoto wao watakavyokuwa baadaye maishani kwa sababu wao ndio wanaowatazama wakikua.

“Malezi ni kama kuwa kocha; unapaswa kufundisha maisha ya mtu; mitandao ya kijamii ni maisha yao; hiyo ni sehemu ya maisha inabidi uanze kwenda nao, kama umemshikilia.

Aliwataka wazazi kuwafundisha watoto wao kuweza kukabiliana na kukosolewa hadharani kwa sababu, wakati fulani maishani wanaweza kukabiliwa na mambo hayo, na kuwafundisha mapema kutawasaidia wasiingie kwenye msongo wa mawazo.

“Wafunze watoto wako kuweza kushughulikia mambo mazuri na mabaya. Ni muhimu sana kwa sababu huwezi kumlinda mtu kupita kiasi, mpaka hawezi kujishughulikia, inapotokea kitu kama chuki.” Nameless alishiriki chapisho.