Elsa Majimbo awajibu wanaodai kuwa ‘matajiri hawajisifu’

Ni kwamba tu vitu wanavyojisifu sio unavyojisifu. Hawazungumzi kuhusu Gucci; wanazungumza kuhusu nyumba na magari

Muhtasari

•Unajua ninachokiona ni cha kuchekesha  wakati watu kwenye mtandao wanakuja hapa kuniambia jinsi watu matajiri wanavyofanya na kutokuwa na tabia.

•Namaanisha, ungejuaje? Ndiyo wanafanya. Ni kwamba tu vitu wanavyojisifu sio unavyojisifu nazo.

Image: INSTAGRAM// ELSA MAJIMBO

Mtayarishaji wa maudhui kutoka Kenya Elsa Majimbo amejibu watu wanaomkashifu kuwa matajiri hawajisifu.

Alijibu watu akisema kuwa matajiri hawajisifu, akifafanua kuwa matajiri hujisifu; ni vile wanajisifu kwa mambo tofauti na watu wengine.

"Unajua ninachokiona ni cha kuchekesha  wakati watu kwenye mtandao wanakuja hapa kuniambia jinsi watu matajiri wanavyofanya na kutokuwa na tabia.

Namaanisha, ungejuaje? Ndiyo wanafanya. Ni kwamba tu vitu wanavyojisifu sio unavyojisifu nazo. Hawazungumzi kuhusu Gucci; wanazungumza kuhusu nyumba na magari—mambo ambayo yako katika kiwango tofauti.” Majimbo alisema.

Hivi majuzi aliwaambia mashabiki wake kwamba hahitaji pesa zao kwa sababu yuko vizuri na angetaka maudhui yake yawe ya shughuli ambayo utahitaji kulipa ili kutumia.

“Wengine mnajaribu kunitumia pesa, nadhani ni zawadi, na mnataka nikubalie maombi yenu ili nipate pesa kutoka kwenu.

Tusifanye hivyo, jamani. Tusijaribu kutuma pesa. Tusifanye zawadi. Sitaki hiwe hivo, hasa inapokuja kwa maudhui ambayo ninachagua kushiriki nanyi. Kila mtu yuko hapa kwa sababu amechagua kuwa hapa. Usiharibu hilo." Elsa alisema.