“Mwacheni a’enjoy ujana, bado ni bikira!” Nandy amtetea Yammi kuvaa nguo tumbo-wazi

Nandy anahisi wengi wanaoonesha chuki dhidi ya mavazi ya Yammi ndio wale wale wanaopigia saluti mavazi ya wasanii wa ughaibuni kama vile kina Rihnanna, Beyonce na wengine.

Muhtasari

• "Mnakerekaga pia mkiwaona kina ayra, tyla, tiwa, beyonce na wengine wengiii... haya basi tusifike mbali mbona hapa TZ wasanii wengi wa kike wanaonyesha matumbo yao flat mazuri," alisema Nandy.

Yammi, msanii wa lebo ya African Princess
Yammi, msanii wa lebo ya African Princess

Bosi wa lebo ya muziki ya African Princess, Nandy amejitokeza na kumkingia kifua msanii wake, Yammi dhidi ya maneno makali kutoka kwa baadhi ya watumizi wa mitandao ya kijamii kisa uvaaji wake wanaodai si wa stara.

Kupitia ukurasa wa Instagram, Nandy alichapisha video ya Yammi akiwa anaserebuka katika moja la vazi la mtindo huo wa kuonesha tumbo wazi na kumtetea akisema kwamba bado ni kijana na anafaa kuachwa ili uufurahia ujana wake.

Nandy pia alifichua kwamba kando na Yammi kufurahia ujana wake, yeye bado ni bikira na ana kila haki ya kujivinjari maisha yake ya ujana kwa mitindo ya mavazi ainati kabla ujana haujayeyuka, kwani ni kama moshi.

“Kwanza kabisa yammi vile alivo ndiyo yeye!! Kwanza bado bik..r na mdogo sana mwacheni a enjoy ujana wake! THAT HER BRAND na kiukweli anabaruza haswaaa 🙌🏽 tuvumilie tu sisi wenye majaba tupunguze hasira, me mwenyewe nikipata flat tummy aaaah mmekwisha, haya tuendeee ku enjoy LONELY TUNAWAPENDA,” Nandy alisema.

Vile vile, bosi huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja na mpenzi wa msanii Billnass alisema kwamba wengi wanaoonesha chuki dhidi ya mavazi ya Yammi ndio wale wale wanaopigia saluti mavazi ya wasanii wa ughaibuni kama vile kina Rihnanna, Beyonce na wengine.

“Ila in serious note mashabiki zangu na mashabiki wa yammi naona wanawake weeeengi wakimtukana yammi kufunika tumbo lake why? Mnakerekaga pia mkiwaona kina ayra, tyla, tiwa, beyonce na wengine wengiii... haya basi tusifike mbali mbona hapa TZ wasanii wengi wa kike wanaonyesha matumbo yao flat mazuri 😎 shida ni kuonyesha au shida ni hatuna matumbo yao tunakuwa attacked direct 😂!” Nandy alisema.

Maoni yako ni yepi kuhusu mtindo wa mavazi ya msanii Yammi TZ?