Mwanahabari Fred Muitiriri aeleza jinsi ghafla aliambiwa kazi imeisha

Ulipaswa kutufuta kazi mnamo Julai; unawezaje kufunga kituo cha televisheni mnamo Desemba?

Muhtasari

•Fred Muitiriri, mtangazaji wa NTV, akiri kwa mzaha kufutwa kazi wakati wa sikukuu za Krismasi.

•Akisimulia hadithi yake kwa kicheko, Muitiriri alisema waliitwa kwenye mkutano kuhusu kampuni yao kufungwa.

•Alifichua pia kwamba tukio la kufutwa kazi lilikuja mara tu baada ya janga la COVID-19.

Fred Muitiriri
Image: Facebook

Fred Muitiriri aeleza jinsi kazi ilivyoisha katika kituo kimoja cha televisheni wakati wa Sherehe za Desemba.

Mwanahabari wa NTV Fred Muitiriri ameeleza jinsi alivyopoteza kazi yake katika kituo cha hicho baada tu ya janga la COVID-19 na alipokuwa karibu kusherehekea Krismasi.

Katika video ya kusisimua aliyoweka  kwenye mtandao wake waTikTok, Muitiriri alisema waliambiwa kituo chao kingefungwa katika mkutano.

“Hata nilichelewa kufika kwenye mkutano huo na nikamuuliza mwenzangu  kinachoendelea, naye akafoka akisema kituo kilikuwa kinafungwa," mtangazaji huyo alisema huku  akicheka.

Alifichua pia kwamba tukio la kufutwa kazi lilikuja mara tu baada ya janga la COVID-19 a alipokuwa karibu kusherehekea Krismasi.

"Ulipaswa kutufuta kazi mnamo Julai; unawezaje kufunga kituo cha televisheni mnamo Desemba? Hata hatukuwa tumepona kutokana na janga la COVID-19," aliongeza.

Muitiriri alieleza kuwa kazi hio iliisha  ndani ya muda mfupi.

Wakenya walitoa maoni kufuatia video hio:

Sophie Navutete:

 "Umeteseka kwa dunia lakini Mungu ni mwaminifu"

sherryadvica1:

"Woiiee nimekupata nimeelewa...aki hawakutenda mema."

Essy Kuria:

"Woiii atleast sahii unacheka todu weeeh Christmas hakika na mipango ya kwenda ushago kuuza hofu."

@kakuhRuth:

 "Aaah ni kicheko kwangu.”

Juls Wairimu:

"You missed a lot if ulikuja baadae.Mimi nilikuwa nimekuja morning shift."

Director Mokaya:

"Waliamua December kila mtu akule kwao."