Kwa nini Prince Indah amesitisha uzinduzi wa filamu yake ya ‘Kienyeji’ na Samidoh

Uzinduzi wa filamu ya Prince Indah na Samidoh ulikuwa utokee siku moja tu baada ya wenzao, Bahati na mkewe Diana Marua kuzindua kipindi chao cha uhalisia kwenye jukwaa la Netflix.

Muhtasari

• Uzinduzi wa filamu ya Prince Indah na Samidoh ulikuwa utokee siku moja tu baada ya wenzao, Bahati na mkewe Diana Marua kuzindua kipindi chao cha uhalisia kwenye jukwaa la Netflix.

Prince Indah na Samidoh wametoa wimbo mpya 'Bado Nakupenda'
Image: INSTAGRAM// SAMIDOH

Wakenya wapenzi wa filamu za humu nchini wamebaki katika njia panda baada ya msanii wa Ohangla, Prince Indah kutangaza kusitishwa kwa uzinduzi wa filamu yake na msanii wa Mugithi, Samidoh kunako dakika za mwisho.

Filamu yao wawili hao kwa jina ‘Kienyeji’ ilitarajiwa kuzinduliwa leo Jumamosi ya Juni 8 lakini saa chache tu kuelekea siku ya ndovu kumla mwanawe, Prince Indah alitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram kwamba zoezi hilo la uzinduzi wa filamu halitofanyika tena.

Aidha, Inda alisema kwamba kusitishwa kwa uzinduzi wa filamu yao ni kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wao.

Notisi hiyo ilisoma;

“Tunasikitika kuwataarifu kuwa KIENYEJI FILM PREMIERE ambayo ilipangwa kesho tarehe 8 JUNE 2024 imekuwa imeghairiwa.

Tunafahamu matarajio mengi ya tukio hili lakini hatua hii ilitokana na hali zisizoweza kuepukika. Sisi na wengine wa kamati ya maandalizi hatukuwa na chaguo ila kuchukua mwelekeo huu, kughairi.

Pia tunasikitika kwa usumbufu wowote unaoweza kukusababishia. Kwa wale ambao tayari walikuwa wamelipia tikiti, maelezo yako ya malipo kutoka kwa madfun.com yatarejeshwa mara moja na kurejesha pesa kwa ufanisi.

Kwa mara nyingine tena, asante kwa usaidizi wako usioyumbayumba, tuna imani kubwa kuwa Waziri Mkuu atafanyika hivi karibuni.

Wakati huo huo, tunayofuraha kuwakaribisha #TeamJanabi kwenye NYADHI FESTIVAL ndani ya CARNIVORE GROUNDS, mjitokeze kwa wingi ili tumuunge mkono kaka yangu JOHNNY JUNIOR kwa pamoja.”

Uzinduzi wa filamu ya Prince Indah na Samidoh ulikuwa utokee siku moja tu baada ya wenzao, Bahati na mkewe Diana Marua kuzindua kipindi chao cha uhalisia kwenye jukwaa la Netflix.

Samidoh na Prince Indah ni marafiki wa muda mrefu na mwaka jana walifanikisha kuachia kolabo ya pamoja kwa jina ‘Bado Nakupenda’ ambayo ilileta pamoja lugha za Kikuyu na Luo kwenye utunzi.