Mke wa Presenter Ali ataja sharti la kutimizwa ili kupata watoto zaidi

"Sijali kuzaa watoto wengi iwezekanavyo, wenye Mungu atanibariki nao, mradi kila mtoto aje na Benz," alisema.

Muhtasari

• Madina alisema yeye hajali kuzaa watoto zaidi mradi kuwe na gari aina ya Mercedes-Benz kama zawadi.

•Medina pia alieleza kwa nini amekuwa hashiriki kwenye chaneli yake ya YouTube.

Presenter Ali na Madina
Image: Instagram KWA HISANI

Mke wa Presenter Ali, Medina, amezungumzia sharti moja ambalo angehitaji mumewe atimize ili apate watoto zaidi.

Akizungumza katika uzinduzi wa shoo ya The Bahati's Empire, Madina alisema yeye hajali kuzaa watoto zaidi, na hakikisho pekee aliloomba kwa mwanaume wake ni kwamba kwa kila ujauzito anaoupata, kuwe na gari aina ya Mercedes-Benz kama zawadi.

"Sijali kuzaa watoto wengi iwezekanavyo, wenye Mungu atanibariki nao, mradi kila mtoto aje na Benz." Madina alisema.

Medina pia alieleza kwa nini amekuwa hashiriki kwenye chaneli yake ya YouTube, akisema aliamua kupumzika kidogo na kumpa mtoto wake umakini, lakini atarejea.

Kuwa mama hakika ni sehemu ngumu. Ilinibidi nipumzike ili kumtunza binti yangu kwa sababu nilitaka kumpa uangalifu kamili, halafu sasa wakati wa mtoto unapofika, ndivyo hivyo na kwa njia nyingine karibu wakati wa kazi.

Kama ilivyo sasa, nimerudi kwenye YouTube, lakini nilitaka sana kuchukua mapumziko kidogo ili kushughulikia mambo nyumbani kwanza.Madina alieleza.