'Maadui wangu hawatashinda kamwe,' Karen Nyamu afurahi baada ya kurejesha akaunti yake ya WhatsApp

Akaunti yake ilipigwa marufuku kwa sababu ya kupokea jumbe nyingi.

Muhtasari
  • Sakata zima ilianza pale mawasiliano ya viongozi wa serikali yalipovuja. Hatua hiyo ililenga kuwashawishi viongozi kukataa Mswada wa Fedha ulipowasilishwa bungeni.
KAREN NYAMU
KAREN NYAMU
Image: HISANI

Seneta mteule Karen Nyamu ana furaha baada ya kufanikiwa kurejesha Akaunti yake ya WhatApp.

Kwenye simulizi yake ya Insta, Nyamu alisema kuwa ana kibali cha Mungu na ndiyo maana huwa na kichwa ngumu kila wakati.

Aidha aliwataka wafuasi wake kuendelea kumtumia pesa wanapothibitisha utambulisho wake.

“WhatsApp yangu imerudi hehehe. Maadui zangu hawatashinda kamwe. Me ni kalastborn ka God ndio maana nina kichwa ngumu. Pesa zimuok kumuok. 5 bob kwenda juu,” alisema.

Hapo awali Karen Nyamu alikuwa ametumia akaunti yake ya Instagram kushiriki masikitiko yake baada ya kupoteza akaunti yake ya WhatsApp.

Akaunti yake ilipigwa marufuku kwa sababu ya kupokea jumbe nyingi.

"Licha ya kunitumia 1ksh na 5 ksh nyingi unaweza kuona kile ambacho kunitumia meseji mara kwa mara kwenye WhatsApp kumefanya tuture ,mume furahi sasa siwezi chat sindio?," Nyamu aliandika.

Sakata zima ilianza pale mawasiliano ya viongozi wa serikali yalipovuja. Hatua hiyo ililenga kuwashawishi viongozi kukataa Mswada wa Fedha ulipowasilishwa bungeni.

Karen Nyamu hata hivyo aliweka wazi kwamba anaunga mkono Mswada wa Fedha na akaendelea kutoa matamshi yasiyojali.

Nyamu alikasirisha Wakenya wengi baada ya kusema hajali kuhusu sodo kutozwa ushuru kwa vile hata hazitumii.

Mama huyo wa watoto 3 alishiriki haya alipokuwa katika mijadala mikali na wanamtandao wakimpigia debe kutetea mswada huo.

"Kwa nini isiwe hivyo? Kampuni nyingi sana za Kichina tayari zinatengeneza hapa kile tunachoagiza. Angalau kazi na malighafi ni yetu,” alihoji