Zari asherehekea mtoto wa ujana wake kufikisha miaka 21, ashauri warembo kutoavya mimba

“Wasichana, huyo mwanamume unayehangaikia kuavya mimba zake ana wasichana wengine 5 wanaofanya hivyo.... Katika siku zijazo, utataka kutulia na kupata watoto, na haitawezekana. Tumia mipira ya kinga au mzae mtoto wako....

Muhtasari

• Zari mwenye umri wa miaka 43 na mama kwa watoto watano alimpata mwanawe akiwa na umri wa miaka 22.

• Aliwashauri mabinti kutoavya mimba zinazotokea ghafla katika umri wao mdogo, akisema kwamba kuendelea kuavya mimba ukiwa mdogo ukifika ukubwani utatamani mtoto na hutapata.

ZARI NA MWANAWE WA MIAKA 21.
ZARI NA MWANAWE WA MIAKA 21.
Image: INSTAGRAM

Zari Hassan ni mama mweye furaha baada ya mwanawe aliyempata katika umri mdogo kufikisha umri wa miaka 21.

Kupitia Instagram yake Zari alichapisha picha za mwanawe wa kwanza kwa jina Pinto Tlale na kuonyesha furaha ya uamuzi wake wa kutoavya mimba yake kwani aliipata akiwa katika umri mbichi zaidi.

Zari mwenye umri wa miaka 43 na mama kwa watoto watano alimpata mwanawe akiwa na umri wa miaka 22.

Aliwashauri mabinti kutoavya mimba zinazotokea ghafla katika umri wao mdogo, akisema kwamba kuendelea kuavya mimba ukiwa mdogo ukifika ukubwani utatamani mtoto na hutapata.

Hapa tupo miaka 21 baadaye. Nakupenda, @pinto.tlale, na heri ya siku ya kuzaliwa,” Zari alichapisha.

Aliwashauri wasichana kutohadaiwa na wanaume kuavya mimba zinazotokea katika umri mchanga akisema kwamba ni heri kutumia kinga au kuchukua maamuzi ya kujifungua mtoto wako ikishatokea kwamba umepata ujauzito.

“Wasichana, huyo mwanamume unayehangaikia kuavya mimba zake ana wasichana wengine 5 wanaofanya hivyo.... Katika siku zijazo, utataka kutulia na kupata watoto, na haitawezekana. Tumia mipira ya kinga au mzae mtoto wako....” alisema.

Zari alisema kwamba mtoto kifunguamimba siku zote huwa wa kumpa mwanamke yeyote masomo mengi katika maisha ambayo hakuna darasa linalofunza.

“Muda wote huwa wanasema wazaliwa wa kwanzani mtu ambaye anapitia yote akiwa na wewe, mimi kabisa nakubaliana,” aliongeza.