Ndoa ya Thee Pluto na Felicity Shiru yavunjika baada ya miaka 3

“Tutaendelea kushirikiana vizuri kwa ajili ya malezi ya binti wetu ili asije akathurika. Tupeni muda wakati huu tunapitia mgumu, ahsanteni,’ Pluto alimaliza.

Muhtasari

• Kupitia Instagram, Pluto alichapisha ujumbe akithibitisha kusambaratika kwa ndoa yake iliyodumu kwa miaka 3.

• Aliomba mashabiki wake kuheshimu faragha yao wakati huu ambapo kila mmoja wao ameamua kujishughulisha na hamsini za kwake.

THEE PLUTO NA FELICITY SHIRU
THEE PLUTO NA FELICITY SHIRU
Image: INSTAGRAM

YouTuber Thee Pluto ametangaza kuvunja uhusiano wake wa kimapenzi na mpenzi wake Felicity Shiru.

Kupitia Instagram, Pluto alichapisha ujumbe akithibitisha kusambaratika kwa ndoa yake iliyodumu kwa miaka 3.

Aliomba mashabiki wake kuheshimu faragha yao wakati huu ambapo kila mmoja wao ameamua kujishughulisha na hamsini za kwake.

‘Tumeamua kila mmoja kufuata njia yake na hivyo kufikisha mwisho uhusiano wetu uliodumu kwa miaka mitatu. Ahsante kwa sapoti yenu kutoka kwa familia, marafiki na mashabiki. Hebu na tusije tukaanza kushuku chochote na kuanza kusambaza uvumi usio wa kweli kuhusu utengano wetu,” Thee Pluto alitangaza.

Aidha, baba huyo wa mtoto mmoja wa kike, Zoey alisema kwamba licha ya kutalikiana, wataendelea kushirikiana sako kwa bako kwa ajili ya maleiz ya binti wao.

“Tutaendelea kushirikiana vizuri kwa ajili ya malezi ya binti wetu ili asije akathurika. Tupeni muda wakati huu tunapitia mgumu, ahsanteni,’ Pluto alimaliza.

Taarifa hizi za kuvunja moyo zinajiri siku chache tu baada ya Pluto kumsherehekea mpenzi wake kwa ujumbe mtamu mitandaoni wakati wa siku yake ya kuzaliwa.

‘Mama kwa binti yangu, ninathamini uhusiano ambao tumeunda pamoja, kubadilishana upya kujitolea kwetu kwa uhusiano wetu wakati wa siku yako ya kuzaliwa ni tamaduni nzuri na inaashiria kujitolea kwetu kudumisha uhusiano wetu pamoja. Ninajivunia muda ambao tumekaa pamoja na natazamia kuishi miaka mingi ya furaha pamoja,” sehemu ya ujumbe wa Thee Pluto kwa mkewe ulisomeka siku 3 zilizopita.