Rema awataka mashabiki wa Afrobeats kumpa maua yake, “Tayari nimehimiza kizazi kijacho!”

Pia alitetea kauli yake kwamba sasa hivi Afrobeats si kuhusu wasanii wakuu watatu – Wizkid, Davido na Burna Boy bali sasa wamefika wanne, yeye akiwa kwenye orodha hiyo.

Muhtasari

• Pia alitetea kauli yake kwamba sasa hivi Afrobeats si kuhusu wasanii wakuu watatu – Wizkid, Davido na Burna Boy bali sasa wamefika wanne, yeye akiwa kwenye orodha hiyo.

• Hitmaker huyo pia alibainisha kuwa haipaswi kuwa na miaka 30 kabla ya kupewa maua yake kama mwimbaji wa Afrobeat.

Image: Screengrab//YT

Msanii wa Nigeria, Divine Ikubor, maarufu kwa jina la Rema, amewataka wapenzi wote wa muziki wa Afrobeats kutambua mchango wake katika muziki huo na kumpa maua yake, miaka 3 tu baada ya kuvuma, shukrani kwa kibao chake cha ‘Calm Down’.

Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini Nigeria, Rema alisema kwamba katika kipindi kifupi ambacho amekuwa kwenye Sanaa ya muziki, tayari amehimiza pakubwa kizazi kijacho cha muziki na kuwaambia mashabiki na washikadau wa muziki kwamba si lazima wasubiri afikishe miaka 10 kwenye muziki ili kutambua mchango wake.

Pia alitetea kauli yake kwamba sasa hivi Afrobeats si kuhusu wasanii wakuu watatu – Wizkid, Davido na Burna Boy bali sasa wamefika wanne, yeye akiwa kwenye orodha hiyo.

Hitmaker huyo pia alibainisha kuwa haipaswi kuwa na miaka 30 kabla ya kupewa maua yake kama mwimbaji wa Afrobeat.

“Mchango wangu kwa safari ya muziki wa Afrobeats kuenda kote duniani ni kubwa. Sasa hatupaswi kuzungumzia kuhusu Big 3, ni Big 4 sasa. Tuzo ainati ambazo zimetolewa zimeunda kategoria hii kutokana na ufanisi wa muziki wangu. Nilifanya balaa katika miji mitatu nchini India na Wahindi walinishabikia pakubwa. Hivyo, lazima nifikishe umri wa miaka 30 ndio nipewe maua yangu? Nyakati zimebadilika,” Rema alisema.

Katika video hiyo, staa huyo wa muziki aliyetumbuiza nchini Benin, jimbo la Edo alieleza kuwa mchango wake kwenye Afrobeat umekuwa mkubwa, na haikuwa kuwa na wimbo uliohit pekee.

Rema alitaja jinsi India ilimpokea na kuimba nyimbo za Afrobeat.

Pia aliongeza kuwa aliweza kuunda kitengo cha Afrobeat katika tuzo kwa sababu ya mafanikio yake katika aina hiyo.