Muundaji maudhui Iam_marwa afichua anataka watoto 10

“Ndiyo,tunataka familia kubwa, watoto 10, kwa hivyo haraka iwezekanavyo tunataka watoto wetu wakue pamoja," Marwa aliandika.

Muhtasari

•Mapema mwaka huu alitangaza kuwa mkewe Ro Cabrera ni mjamzito na kuwa mtoto wao atazaliwa Argentina

•Walipatana na Ro kupitia app ya kuchumbiana ya 'Bumble'

Fredrick Marwa,Ro Cabrera
Fredrick Marwa,Ro Cabrera
Image: Fredrick Marwa//Facebook

Muundaji wa maudhui Fredrick Marwa almaarufu iam_marwa anasema anataka watoto kumi.

Akijibu swali la shabiki wake ambaye aliuliza ni lini anataka kupata mtoto wa pili, Marwa alisema yeye na mkewe wanataka familia kubwa na watoto 10 na kuwa watapata mtoto wa pili hivi karibuni kwa kuwa wanataka watoto wao wakue pamoja.

Ndiyo,tunataka familia kubwa...Kwa kweli watoto 10, kwa hivyo haraka iwezekanavyo tunataka watoto wetu wakue pamoja...Nampenda baba mkwe wangu sana yeye ndiye ninachotamani kabisa,”Marwa aliandika.

Marwa na Rocio Cabrera walitangaza ujauzito wa mtoto wao wa kwanza mapema mwaka huu na wakasema kuwa mtoto wao atazaliwa Argentina.

Marwa alieleza kuwa walikutana na mkewe Ro Cabrera kupitia app ya kuchumbiana ‘Bumble’. Alikuwa akisafiri Mexico na alijiunga na app ya kuchumbiana ambapo aliunganishwa na Ro.

Nilikuwa Mexico na nikaamua kujaribu Bumble. Mwanamke ndiye anatuma meseji wa kwanza, Rocio alituma ujumbe akisema hi,” Marwa alisema.

Siku hiyo hiyo walikutana na kupata chakula cha mchana pamoja.

Alikuwa akitafuta mtu ambaye wangesafiri pamoja

"Nilikuwa natafuta mwenza wa kusafiri ambaye anapenda kuchunguza," alisema.

Marwa pia alisema kuwa alipendezwa na Rocio alipomwona.

“Alikuwa anavutia sana, yeye kutokuwa mwenyeji wa Mexico ilionyesha kuwa tayari ameshaiona dunia.” Marwa aliongeza.

Marwa ni Youtuber na mwanablogu wa kusafiri ambaye husafiri kote ulimwenguni.

Wanatarajia mtoto wao wa kwanza pamoja ambaye atazaliwa Novemba.

Kwa sasa wako Argentina na familia ya Rocio.