Dlamini Nkululeko maarufu kama ‘King of Squats’ yuko nchini Kenya kutoa mafunzo ya gym

Anajulikana sana kwa mapaja yake na mara nyingi huwavutia watu wanaopenda mazoezi ya viungo kupitia mazoezi ya mwili ambayo hulenga zaidi squats.

Muhtasari

• Nkululeko alianza kutoa mafunzo kwa mwana na mke wa mfalme wa Swaziland na mara baada ya hapo kukaja kuzaliwa kwa mazoezi yake maarufu.

Dlamini Nkululeko
Dlamini Nkululeko
Image: HISANI

Dlamini Nkululeko, raia wa Afrika Kuisni maarufu kama King of Squats katika mitandao ya kijamii yumo nchini Kenya kwa ajili ya muendelezo wa mafunzo kwa wapenzi wa mazoezi ya gym jinsi ya kufanya mazoezi ya kuinama na kuinuka.

Nkululeko, maarufu kwa umbile lake kama la kike hali ya kuwa yeye ni mwanamume amekuwa gumzo la mitandaoni kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na jinsi anavyofanya mazoezi yake, haswa na wanawake.

Mtaalamu huyo wa mazoezi ya viungo, ambaye alijipatia umaarufu mkubwa mwaka wa 2023, anajulikana sana kwa mapaja yake na mara nyingi huwavutia watu wanaopenda mazoezi ya viungo kupitia mazoezi ya mwili ambayo hulenga zaidi squats.

Katika mahojiano ya awali, Nkululeko alisema ndoto yake ya awali ilikuwa kuwa mchezaji wa soka wa kulipwa na hata kuwindwa na baadhi ya klabu zinazoongoza katika mji aliozaliwa.

"Safari yangu ya utimamu ilianza na soka. Nilikua nikicheza soka nyumbani na ndoto yangu ilikuwa ni kuishia kuwa mchezaji wa kulipwa.

Baadaye alifuatwa na Amazulu na Jomo Cosmo lakini akasajiliwa na hao wa pili. Nkululeko hakupata nafasi za kutosha za kuonyesha umahiri wake mbele ya lango na baada ya kukaa Eswatini, aliamua kujitosa kwenye kile alichokipenda, utimamu wa mwili.

 

Nkululeko alianza kutoa mafunzo kwa mwana na mke wa mfalme wa Swaziland na mara baada ya hapo kukaja kuzaliwa kwa mazoezi yake maarufu.