"sina shida akitexti wanadada wengine" - Ikoh Roz

Mrembo ambaye wengi wamedai kuwa ni mpenzi wa msanii Willy Paul, Iko Roz amsema kwamba haoni shida mpenziwe akiwatexti wanadada wengine.

Muhtasari

•Mrembo amabaye ukisiwa wako kwenye mahusiano na msanii wa ngoma za kizazi kipya Willy Pozee,Ikoh Roz asema yuko sawa na mpenziwe akiwatexti wanadada wengi borake anamjali.

IKOH ROZ//WILLY POZEE
Image: HISANI

Mrembo ambaye wengi wamedai kuwa ni mpenzi wa msanii Willy Paul, Iko Roz amsema kwamba haoni shida mpenziwe akiwatexti wanadada wengine. 

Kupitia mahojiano na bloga mmoja,kipusa huyo alidokeza kuwa ni jambop la kwaida mwanaume 'kudm' wanadada.

"kitu kimoja najua ni kwamba na ambacho ni cha kwaida,ni kuwa utapata mwanaume wako aki Dm,wanadada lakini kikubwa wanataka kutrendi na kiki katika tiktok juu ya Willy Paul.swali,ni mara ngapi hao wanadada upata 'dms' lakini utawaona tuu wakipostii za Willy Paul" . Mrembo huyo alisema.

Aidha,Ikoh alisema kuwa Pozzeh ndiye anafaa kuachana na hiyo tabia ila yeye mwenyewe haoni kama anaeza mbadilisha.Vinginevyo,alieleza kuwa ako na shida na mpenziwe kwa kuwa yeye kila mara yupo na wanadada wengine wakati wapo pamoja.

Kufuatia matamshi yake Ikoh,ni jambo ambalo liliwaacha wafuasi wa mtandao huo na hisia mseto baada ya yeye kuonekana ametamauka na mahusiano hayo na msanii huyo.

Ikimbukwe ni siku chache zilizopita baada ya msanii huyo aleyetunga kibao cha Saldido kusema anamtafuta mtoto wa kike na wasishangae akiingia dm.

Pozee, kama anavyojiita alichapisha ujumbe kwenye Instastory,mda wa hapo awali  akisema kwamba msichana yeyote ambaye ni mrembo kupindukia na anatumia mtandao wa Instagram, asishangae atakapomuona kwenye DM yake.

“Wewe ni mwanamke mrembo sana? Model type? Sawa, nitarajie kwenye DM yako mimi mwenyewe. Hivyo, ukiniona ninakuomba namba yako usishangae, niko na kazi kwako,” Pozee alichapisha.