Auntie Jemimah asema kuwa anaogopa mapenzi

licha ya kuwa ameona ndoa zilizonawiri, kwake binafsi hajaweka maswala ya kuingia katika ndoa kamaswala muhimu

Muhtasari

• Kwa mara kadhaa sasa Auntie Jemimah amesisitiza kuwa mapenzi kwake si kipaombele.

Image: HISANI

Mchekeshaji maarufu Auntie Jemimah amesema kuwa hajaweka maswala ya ndoa kama kitu chenye kipaombele katika maisha yake.

Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha habari cha mtandaoni, Auntie Jemimah amesema kuwa anaogopa ndoa sana.

Aidha, licha ya kuwa ameona ndoa zilizonawiri, kwake binafsi hajaweka maswala ya kuingia katika ndoa kamaswala muhimu sana linalohitaji kuwekwa kipaombele.

"Ndoa huwa si kitu cha kipaombele, naogopa ndoa sana." Alisema Auntie Jemimah.

Mchekeshaji huo ambaye pia ni muigizaji amekiri kuwa yuko sawa ikiwa itatokea kwake na kama ikiwa pia haitatokea katika maisha yake bado ni sawa.

Auntie pia amesisitiza kuwa hajaweka mawazo yake kuwa katika mahusiani na hata kukosa kuwa katika ndoa sdi jambo linaloweza kumfanya ajiue.

Mtangazaji huyo wa zamani wa Gukena FM, katika mahojiano kadhaa, mara kwa mara amekuwa akisisitiza kuwa hayuko tayari kwa mswalaya ndoa.

Mwaka jana, Auntie Jemimah kwenye podikasti moja ya humu nchini,alitoa sababu kuwa akiingia katika ndoa, mambo mengi ambayo hajatimiza yatakosa kutimia.